Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji

SERIKALI YAKABIDHI PAMPU 52 ZA UMWAGILIAJI WAKULIMA KATAVI KUONGEZA TIJA NA KULINDA MAZINGIRA

Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imekabidhi pampu 52 za umwagiliaji zenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 500 kwa vikundi 46 vya wakulma wa Mkoani Katavi, ikiwa ni hatua ya kuongeza tija, kupanua eneo linalolimwa na kuimarisha usalama wa chakula. Hafla hiyo ya ugawaji imefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, ambapo mkoa huo umekuwa miongoni mwa wanufaika wa awamu ya kwanza ya mpango huo wa kuimarisha matumizi ya teknolojia ya umwagiliaji katika kilimo nchini.

slot gacor