Dira na Dhima
Dira
Kuwa kitovu cha umahiri katika kutoa utaalamu wa huduma za umwagiliaji nchini.
Dhima
Kuhamasisha, kuratibu na kudhibiti maendeleo ya umwagiliaji ili kuleta ufanisi na umwagiliaji endelevu nchini.
Malengo ya Tume
Lengo kuu la Tume ni kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wa maji kwa ajili ya umwagiliaji kwa kuzingatia matumizi bora ya maji katika umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji wa mazao wenye tija kwa maendeleo ya uchumi wa Taifa.
Katika kufanisha hayo Tume inatekeleza Malengo Mahususi yafuatayo:-
- Kuchochea uwekezaji wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kwenye kilimo cha umwagiliaji;
- Kuhakikisha kuwa Mfuko wa Maendeleo ya Umwagiliaji unafanya kazi kwa mujibu wa sheria;
- Kuhamasisha matumizi bora ya maji katika kilimo cha umwagiliaji;
- Kuhakikisha maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji yanazingatia Mipango Shirikishi ya Rasilimali za Maji;
- Kuhakikisha maendeleo endelevu ya sekta ya umwagiliaji;
- Kuimarisha uwezo wa kitaasisi katika mipango, utekelezajina usimamizi katika ngazi zote;
- Kuwawezesha wanufaika kushiriki kikamilifu katika kupanga, kutekeleza, kusimamia na kuendesha katika ngazi zote za uendelezaji wa umwagiliaji; na
- Kuendeleza na kusambaza teknolojia mpya za umwagiliaji ili kuwezesha matumizi bora ya rasilimali za maji.