Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji

Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Kupitia maafisa ugani wanaopatikana katika kila kata unayoishi

Wasiliana na tume kupitia baruapepe info@nirc.go.tz

NIRC inahusika na kupanga, kuendeleza, na kusimamia mifumo ya umwagiliaji nchini. Pia huhakikisha matumizi endelevu ya umwagiliaji, hutoa msaada wa kitaalamu kwa wakulima, na kuhimiza matumizi ya teknolojia za kisasa za umwagiliaji.

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ni Taasisi ya Kiserikali iliyo chini ya Wizara ya Kilimo.

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inatoa elimu ya kilimo cha umwagiliaji kupitia mashamba darasa katika baadhi ya Skimu, ambapo teknolojia mbalimbali za umwagiliaji hutumika. Kwa mkulima anayehitaji kupata taarifa zaidi kuhusu upatikanaji wa teknolojia  za umwagiliaji, huduma hiyo ataipata katika Ofisi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika mkoa wake na Ofisi za tume zilizopo katika baadhi ya wilaya nchini.