Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji

Tunafanya Nini

Majukumu ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

  1. Kuishauri Serikali katika utekelezaji na kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Umwagiliaji, Mkakati wa Maendeleo ya umwagiliaji, Mpango Kabambe wa Taifa wa Umwagiliaji na Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji;
  2.  Kuiwakilisha Serikali kwenye mikutano ya kitaifa na kimataifa katika masuala yote yanayohusu uendelezaji na usimamizi wa kilimo cha umwagiliaji. Kuratibu shughuli zote za umwagiliaji katika sekta ya umwagiliaji zinazotekelezwa na washirika au wadau wengine wa       maendeleo;
  3. Kuhamasisha na kudumisha ushirikiano na taasisi za kimataifa zenye kutekeleza majukumu yanayofanana na Tume katika masuala ya umwagiliaji;
  4. Kupanga, kufanya pembuzi yakinifu, kusanifu, kujenga na kusimamia ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji; 
  5. Kuanzisha na kuendesha vituo vya ukodishaji wa vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kuisaidia sekta binafsi kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji; 
  6.  Kusajili na kutunza orodha ya wamwagiliaji;
  7.  Kuhamasisha na kudumisha mahusiano na taasisi zinazotoa programu za mafunzo na kusaidia upatikanaji wa rasilimali watu kwa madhumuni ya kupata wataalamu katika sekta ya umwagiliaji;
  8. Kuwa jukwaa la kubadilishana uzoefu na kupashana habari katika masuala ya umwagiliaji; Kujenga uwezo wa wamwagiliaji kwa ajili ya kuongeza ushiriki wao katika kupanga, kutekeleza, kuendesha na kusimamia skimu za umwagiliaji; 
  9. Kufanya na kuratibu tafiti, kusambaza teknolojia sahihi zitokanazo na matokeo ya tafiti na kutoa msaada wa huduma za kitaalamu kuhusu umwagiliaji; 
  10.  Kuhamasisha uendelezaji wa mabwawa kwa ajili ya matumizi ya umwagiliaji na shughuli nyinginezo za kiuchumi na kijamii; Kusimamia masuala yote yanayohusu maendeleo ya umwagiliaji na ushirikiano na wadau mbalimbali katika maendeleo ya umwagiliaji;          Kuidhinisha ujenzi wa mifumo ya umwagiliaji, kusimamia viwango na miongozo kwa ajili ya maendeleo na uendeshaji wa shughuli za umwagiliaji; 
  11. Kuhamasisha matumizi ya maji yenye ufanisi katika mifumo ya umwagiliaji na kuhakikisha usimamizi shirikishi wa rasilimali za maji kwa maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji; Kuishauri Serikali katika masuala yote yanayohusu maendeleo na uendeshaji wa sekta ya         umwagiliaji nchini;
  12.  na Kutekeleza majukumu yote muhimu katika kuendeleza kilimo cha umwagiliaji.