Idara ya Uendeshaji
Madhumuni:
Kuhamashisha matumizi ya umwagiliaji na matupio na kutoa usaidizi kwa wadau.
Majukumu ya Idara ni:
- Kuhamasiha matumizi ya fursa za uwekezaji zilizopo, utoaji huduma,utekelezaji wa shughuli za umwagiliaji na matupio;
- Kuwezesha uanzishaji na uimarishaji wa vyama vya wamwagiliaji;
- Kuhamasisha uongozi wa vijiji katika kuunga mkono shughuli za vyama vya wamwagiliaji ili kusimamia na kuendeleza umwagiliaji;
- Kuandaa na kusambaza miongozo ya usimamizi wa vyama vya wamwagiliaji;
- Kuhamasisha matumizi bora ya maji na agronomia katika kilimo cha umwagiliaji;
- Kusaidia mamlaka za Serikali za Mitaa na Vyama vya Wamwagiliaji katika kuandaa na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogo kwa mujibu wa Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji na kanuni zake;
- Kuwezesha uanzishwaji wa mifumo sahihi ya uendeshaji wa skimu ndogo, za kati na kubwa;
- Kuhamasisha matumizi ya umwagiliaji kwa mazao mbalimbali na kwa misimu zaidi ya mmoja.;
- Kuwezesha wakulima wamwagiliaji katika upatikanaji wa huduma za zana za kilimo, pembejeo na huduma za ugani kwa ajili ya uzalishaji mazao wenye tija;
- Kuwezesha wamwagiliaji katika upatikanaji wa teknolojia mbalimbali za kuongeza mnyororo wa thamani ya mazao ili kupata soko zuri lenye kuleta tija.
- Kutoa mchango muhimu katika uandaaji wa sera na mikakati ya kuendeleza umwagiliaji na matupio.
Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi na itakuwa na sehemu mbili zifuatazo:
- Sehemu ya Huduma za Uendeshaji na
- Sehemu ya Huduma za Usaidizi.
- Sehemu ya Huduma za Uendeshaji
Sehemu hii itatekeleza shughuli zifuatazo:-
- Kuhamashisha matumizi ya teknolojia sahihi katika kilimo cha umwagiliaji;
- Kuhamasisha matumizi bora ya maji na agronomia katika kilimo cha umwagiliaji;
- Kuhakikisha kuwa kiasi cha maji yanyopelekwa shambani kinalingana na kibali cha matumizi ya maji kilichotolewa;
- Kutunza na kuhakiki taarifa za uzalishaji mazao kwa ajili ya kubaini mchango wa umwagiliaji kwenye usalama wa chakula;
- Kuwezesha uandaaji wa mipango ya uendeshaji na matengenezo ya skimu za umwagiliaji katika kila mwisho wa msimu na kufanya matengenezo ya mfumo wa umwagiliaji;
- Kuwezesha uandaaji na usimamizi wa ratiba za matumizi bora ya maji shambani;
- Kuwezesha ukusanyaji na matumizi bora ya ada za huduma za umwagiliaji na ada nyinginezo;
- Kuhamasisha matumizi ya umwagiliaji kwa mazao mbalimbali na kwa misimu zaidi ya mmoja.
Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.
3.4.2 Sehemu ya Huduma za Usaidizi
Sehemu hii itatekeleza shughuli zifuatazo:-
- Kuandaa na kusambaza miongozo ya usimamizi wa vyama vya wamwagiliaji;
- Kusaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa kuunda Timu za Wataalamu za kusimamia uendeshaji wa skimu za umwagiliaji;
- Kusaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa na Vyama vya Wamwagiliaji katika kuandaa na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogokwa mujibu wa Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji na kanuni zake;
- Kusaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa kuanzisha na kutunza takwimu za umwagiliaji na kuziunganisha na takwimu za kitaifa;
- Kuwezesha uanzishwaji wa mifumo sahihi ya uendeshaji wa skimu ndogo, za kati na kubwa;
- Kuwezesha wamwagiliaji katika upatikanaji wa teknolojia mbalimbali za kuongeza mnyororo wa thamani ya mazao ili kupata soko zuri lenye kuleta tija
- Kuwezesha uanzishaji na uimarishaji wa vyama vya wamwagiliaji;
Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.