Idara ya Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini
Madhumuni
Kutoa utaalamu na huduma katika mipango, bajeti, ufuatiliaji na tathmini.
Idara hii itafanya kazi zifuatazo:-
- Kuratibu utayarishaji na utekelezaji wa mipango na bajeti ya Tume;
- Kuhamasisha na kuwezesha utoaji huduma kwa sekta binafsi;
- Kutayarisha mchango wa ofisi katika taarifa ya bajeti na taarifa ya kiuchumi ya mwaka;
- Kuweka mfumo wa utayarishaji wa mpango mkakati na kwa kuzingatia ujuzi wa kuandaa bajeti ya Tume;
- Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa sera za Serikali;
- Kufanya uchambuzi wa sera za sekta mbalimbali na kutoa ushauri stahiki;
- Kufanya ufuatiliaji na tathmini katika mipango na bajeti ya Tume na kutayarisha taarifa za utekelezaji;
- Kutafiti, kuchambua na kufanya tathmini ya mipango kwa ajili ya kutoa maamuzi ya mwelekeo wa baadae wa Tume;
- Kuhakikisha kwamba mipango na bajeti ya Tume inajumuishwa katika taratibu za bajeti ya Serikali; na
- Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa miradi / mipango ya maendeleo na upatikanaji wa rasilimali.
- Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi na itakuwa na vitengoviwili kama ifuatavyo:
Kitengo cha mipango; na Kitengo cha Ufuatiliaji naTathmini.
-
- Kitengo chaMipango
Kitengo hiki kitafanya kazi zifuatazo:-
- Kuratibu uandaaji na utayarishaji wa mpango wa mwaka na mpango mkakati wa muda wa kati;
- Kuweka pamoja miradi, mipango, mipango kazi na kuweka mikakati ya upatikanaji wa rasilimali;
- Kuwasiliana na Wizara ya Fedha na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma juu ya michakato ya mipango mkakati na bajeti;
- Kutoa miongozo ya kitaalamu na kusaidia uwepo wa mpango mkakati na bajeti;
- Kushiriki katika uchambuzi wa kazi zisizo za msingi zinazoweza kufanywa na sekta binafsi; na
- Kutayarisha mkataba wa makubaliano kwa miradi na program yenye ufadhili wa kimataifa;
Kitengo hiki kitaongozwa na Mchumi Mkuu
1.2 Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
Kitengo hiki kitafanya kazi zifuatazo:-
- Kufuatilia utekelezaji wa mpango wa mwaka wa Tume pamoja na mpango mkakati wa muda wa kati;
- Kutayarisha taarifa za utekelezaji wa mpango kwa vipindi maalumu (juma, mwezi, robo mwaka, nusu mwaka na mwaka);
- Kukusanya na kuchambua takwimu zinazohitajika katika utayarishaji na utekelezaji wa sera, mipango na mapendekezo ya bajeti;
- Kutoa mchango katika utayarishaji na uaandaji wa mipango na bajeti za Tume ikiwa ni pamoja na kuweka malengo muhimu na viashiria;
- Kutoa usaidizi wa kitaalamu ikiwa ni pamoja na kuweka mfumo wa ufuatiliaji na tathmini;
- Kufanya utafiti wa matokeo ya mipango, miradi na programu mbalimbali;
- Kufanya tathmini ya hali ya utoaji huduma kwa kukusanya maoni ya wadau juu ya huduma zinazotolewa; na
- Kuratibu mapitio ya utekelezaji wa mipango ya nusu mwaka na ya mwaka.
Kitengo hikikitaongozwa na Mchumi Mkuu