Historia

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeanzishwa kwa Sheria Na.04 ya Taifa ya Umwagiliaji ya mwaka 2013 kama Taasisi ya Serikali inayojitegemea chini ya Wizara inayohusika na Umwagiliaji.Tume imepewa mamlaka ya kuratibu,kendeleza na kusimamia Maendeleo ya Sekta ya Umwagiliaji nchini. Shughuli za utendaji za kila siku husimamiwa na Mkurugenzi Mkuu chini ya usimamizi wa bodi yenye wajumbe 10.

1.1 Majukumu ya Tume ya Taifa ya  Umwagiliaji

Majukumu mahususi ya Tume ni kama ifuatavyo:-

  1. Kuishauri Serikali katika utekelezaji na kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Umwagiliaji, Mkakati wa Maendeleo ya Umwagiliaji, Mpango Kabambe wa Taifa wa Taifa wa Umwagiliaji na Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji;
  2. Kuwakilisha Serikali kwenye mikutano ya kitaifa na kimataifa katika masuala yote yanayohusu uendelezaji na usimamizi wa kilimo cha umwagiliaji.
  3. Kuratibu shughuli zote za umwagiliaji katika sekta ya umwagiliaji zinazotekelezwa na washirika au wadau wengine wa maendeleo;
  4. Kuhamasisha na kudumisha ushirikiano na taasisi na kimataifa zenye kutekeleza majukumu yanayofanana na Tume katika masuala ya umwagiliaji;
  5. Kupanga, kufanya pembembuzi yakinifu, kusanifu, kujenga na kusimamia ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji;
  6. Kuanzisha na kuendesha Vituo vya ukodishaji wa vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kuisaidia sekta binafsi kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji;
  7. Kusajili na kutunza orodha ya wamwagiliaji;
  8. Kuhamasisha na kudumisha mahusiano na taasisi zinazotoa programu za mafunzo na kusaidia upatikanaji wa rasilimali watu kwa madhumuni ya kupata wataalamu katika sekta ya umwagiliaji;
  9. Kuwa jukwaa la kubadilishana uzoefu na kupashana habari katika masuala ya umwagiliaji;
  10. Kujenga uwezo wa wamwagiliaji kwa ajli ya kuongeza ushiriki wao katika kupanga, kutekeleza, kuendesha na kusimamia skimu za umwagiliaji;
  11. Kufanya na kuratibu tafiti, kusambaza teknolojia sahihi zinazotokana na matokeo ya tafiti na kutoa msaada wa huduma za kitaalamu kuhusu umwagiliaji;
  12. Kuhamasisha uendelezaji wa mabwawa kwa ajili ya matumizi ya umwagiliaji na shuguli zinginezo za kiuchumi na kijamii;
  13. Kusimamia maswala yote yanayohusu maendeleo ya umwagiliaji na ushirikiano na wadau mablimbali katika maendeleo ya umwagiliaji;
  14. Kuidhinisha ujenzi wa mifumo ya umwagiliaji, kusimamia viwango na miongozo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji;
  15. Kuhamasisha matumizi ya maji yenye ufanisi katika mifumo ya umwagiliaji na kuhakikisha usimamizi shirikishi wa rasilimali za maji kwa maendeleo ya kilimo cha Umwagiliaji;
  16. Kuishauri serikali katika masuala yote yanahusu maendeleo na uendeshaji wa sekta ya umwagiliaji nchini;
  17. Kuendeleza matumizi sahihi ya maji ya umwagiliaji katika mifumo ya umwagiliaji na kuhakikisha kuwa inaendana na usimamizi wa pamoja wa rasilimali za maji katika kilimo cha umwagiliaji;na
  18. Kutekeleza majukumu yote muhimu katika kuendeleza kilimo cha umwagiliaji..      

  1.2 Dira, Dhima na malengo ya Tume

1.2.1 Dira

Kuwa Tume iliyothabiti na yenye uwezo wa kuweka msukumo katika mageuzi ya Sekta ya Umwagiliaji.

1.2.2 Dhima

Kuendeleza miundombinu ya umwagiliaji kwa kuzingatia usimamizi wa pamoja wa rasilimali za maji ili kuleta ufanisi katika matumizi ya maji katika Umwagiliaji kwa lengo la kuwa na uzalishaji na tija endelevu kwa maendeleo ya uchumi wa Taifa.

1.2.3 Malengo ya Tume 

Lengo kuu la Tume ni kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wa maji kwa ajili ya umwagiliaji kwa kuzingatia matumizi bora ya maji katika umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji wa mazao wenye tija kwa maendeleo ya uchumi wa Taifa.

Katika kufanisha hayo Tume inatekeleza Malengo Mahususi yafuatayo:-

  1. Kuchochea uwekezaji wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kwenye kilimo cha umwagiliaji;
  2. Kuhakikisha kuwa Mfuko wa Maendeleo ya Umwagiliaji unafanya kazi kwa mujibu wa sheria;
  3. Kuhamasisha matumizi bora ya maji katika kilimo cha umwagiliaji;
  4. Kuhakikisha maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji yanazingatia Mipango Shirikishi ya Rasilimali za Maji;
  5. Kuhakikisha maendeleo endelevu ya sekta ya umwagiliaji;
  6. Kuimarisha uwezo wa kitaasisi katika mipango, utekelezajina usimamizi katika ngazi zote;
  7. Kuwawezesha wanufaika kushiriki kikamilifu katika kupanga, kutekeleza, kusimamia na kuendesha katika ngazi zote za uendelezaji wa umwagiliaji; na
  8. Kuendeleza na kusambaza teknolojia mpya za umwagiliaji ili kuwezesha matumizi bora ya rasilimali za maji.