Kupata Vifaa vya Umwagiliaji
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inatoa elimu ya kilimo cha umwagiliaji kupitia mashamba darasa katika baadhi ya Skimu, ambapo teknolojia mbalimbali za umwagiliaji hutumika. Kwa mkulima anayehitaji kupata taarifa zaidi kuhusu upatikanaji wa teknolojia za umwagiliaji, huduma hiyo ataipata katika Ofisi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika mkoa wake na Ofisi za tume zilizopo katika baadhi ya wilaya nchini.