Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji

HAFLA YA UZINDUZI NA UGAWAJI VITENDEA KAZI KWA AJILI YA UTEKELZAJI MIRADI YA UMWAGILIAJI

Hafla ya kukabidhia ya vitendea kazi vya miradi ya umwagiliaji iliyofanyika Njedengwa, Dodoma, ikiongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe. Daniel Chongolo. Vifaa hivi vyenye thamani ya Bilioni 23.4 ni sehemu ya mkakati wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) kuongeza eneo la kilimo cha umwagiliaji na kuhakikisha sekta hiyo inachangia asilimia 10 ya ukuaji wa uchumi ifikapo mwaka 2030.