Utawala na Usimamizi wa Raslimali watu

Madhumuni

Kutoa Utaalamu na Huduma ya usimamizi wa rasilimali watu na masuala ya utawala kwa Tume.

Idara hii itafanya kazi zifuatazo:-

(i) Kutoa mapendekezo ya kimkakati kwa uongozi wa Tume juu masuala ya Utawala na usimamizi wa Rasilimali Watu kwa mfano ajira, mafunzo, kupandishwa vyeo, kuhifadhi, kuwapa motisha, upimaji matokeo na maslahi;

(ii) Kuandaa mchakato wa mafao ya kustaafu na malipo ya likizo mbalimbali;

(iii) Kuhakikisha matumizi bora na usimamizi stahiki wa Rasilimali Watu kwenye Tume;

(iv) Kuwa kiungo kati ya Tume ya Umwagiliaji na Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma juu ya utekelezaji wa sera ya Usimamizi wa Utumishi wa Umma na Ajira na sheria zinazoongoza Utumishi wa Umma;

(v) Kutoa takwimu na kuboresha kumbukumbu juu ya taarifa za Rasilimali Watu;

(vi) Kumshauri Mkurugenzi Mkuu juu ya masuala ya Utawala na Rasilimali Watu;na

vi) Kukusanya, kuchambua, kuhifadhi na kusambaza takwimu na taarifa zinazohusu mipango na maendeleo ya Rasilimali Watu.

Idara itongozwa na Mkurugenzi na itakuwa na sehemu mbili kama ifuatavyo:-

(i) Sehemu ya Utawala

(ii) Sehemu ya Rasilimali Watu

1.1 Kitengo cha Utawala

Kitengo hiki kitafanya kazi zifuatazo:-

(i) Kutafsiri na kutekeleza sheria kuu zinazotawala utumishi wa Umma ikiwemo kanuni, Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma, na Sheria nyingine za Kazi;

(ii) Kuwezesha mahusiano kazini na maslahi ya kiutumishi ikiwemo afya, usalama, michezo na utamaduni;

(iii) Kutoa huduma za masjala, kumbukumbu za ofisi, huduma za ofisi na kupeleka na kupokea barua;

(iv) Kusimamia masuala ya kiitifaki;

(v) Kuwezesha utolewaji wa huduma za kiulinzi, usafiri na mambo mengine kwa ujumla;

(vi) Kuwezesha huduma za ujumla za uhifadhi ikiwemo utunzaji wa vifaa vya ofisi, majengo na viwanja;

(vii) Kuratibu utekelezaji wa maadili na kuendeleza ya misingi ya kazi ikiwemo kuzuia rushwa;

(viii) Kutekeleza na kuratibu masuala mtambuka ikiwemo jinsia, ulemavu, UKIMWI n.k.;

(ix) Kusimamia mchakatowa kuboresha utendaji wa kazi;

(x) Kushauri juu ya ufanisi wa utendaji kazi ofisini;

(xi) Kusimamia utekelezaji wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja;

(xii) Kusiammia utekelezaji wa ushiriki wa sekta binafsi katika utoaji wa huduma za ofisi kwa mfano ulinzi, huduma za chakula, usafi, ukarabati wa majengo; na

(xiii) Kuratibu utayarishaji na utekelezaji viwango vya mishahara na ajira.

Sehemu hii itaongozwa na Afisa Tawala Mkuu

1.2 Kitengo cha Rasilimali watu

Kitengo hikikitafanya kazi zifuatazo:-

(i) Kuratibu masuala ya ajira, uteuzi wa wafanyakazi wapya, kupanga vituo vya kazi, kuthibitisha kazini na uhamisho

(ii) Kuwezesha mafunzo ya watumishi na maendeleo ya kazi (maendeleo ya kiutaalamu, kukuza ujuzi, kuboresha utendaji, kustaafu kabla ya muda, mafunzo baada ya muda wa kazi na nje ya nchi);

(iii) Kuwezesha mpango wa mafunzo ya watumishi wapya kazini;

(iv) Kutayarisha mpango wa rasilimali watu kwa kuzingatia upatikanaji na mahitaji ya wataalamu;

(v) Kusimamia mishahara na mchakato wa malipo ya mishahara;

(vi) Kuendesha mchakato wa kuboresha kumbukumbu za likizo mbalimbali kama vile likizo ya mwaka, ugonjwa, uzazi, mafunzo na kustaafu;

(vii) Kusimamia maslahi ya watumishi (kama vile pensheni na posho);

(viii) Kutumika kama sekretareti kwenye kamati ya ajira;

(ix) Kuratibu utekelezaji wa mapitio ya mfumo wa wazi wa matokeo na upimaji wa utendaji kazi (OPRAS), kutathmini matokeo ya upimaji,kuandaa taarifa ya utekelezaji na ufuatiliaji wa ushauri kuhusu fomu za watumishi za OPRAS;

(x) Kuandaa makisio ya mishahara ya Watumishi;

(xi) Kuandaa na kuwezesha utekelezaji wa mpango wa kurithishana madaraka;

(xii) Kufanya tathmini ya mahitaji ya mafunzo na kuandaa mpango wa mafunzo kwa watumishi;

(xiii) Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mpango wa mafunzo wa Tume na kuandaa taarifa ya mafunzo;

(xiv) Kufanya tathmini ya matokeoyampango wa mafunzo na kuandaa tarifa ya tathmini; na

(xv) Kuanzisha na kuratibu kozi za ndani na mafunzo kazini.

Sehemu hii itaongozwa na Afisa Utumishi Mkuu.