Uendeshaji

Madhumuni:

Kuhamashisha matumizi ya umwagiliaji na matupio na kutoa usaidizi kwa wadau.

Majukumu ya Idara ni:

(i) Kuhamasiha matumizi ya fursa za uwekezaji zilizopo, utoaji huduma,utekelezaji wa shughuli za umwagiliaji na matupio;

(ii) Kuwezesha uanzishaji na uimarishaji wa vyama vya wamwagiliaji;

(iii) Kuhamasisha uongozi wa vijiji katika kuunga mkono shughuli za vyama vya wamwagiliaji ili kusimamia na kuendeleza umwagiliaji;

(iv) Kuandaa na kusambaza miongozo ya usimamizi wa vyama vya wamwagiliaji;

(v) Kuhamasisha matumizi bora ya maji na agronomia katika kilimo cha umwagiliaji;

(vi) Kusaidia mamlaka za Serikali za Mitaa na Vyama vya Wamwagiliaji katika kuandaa na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogo kwa mujibu wa Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji na kanuni zake;

(vii) Kuwezesha uanzishwaji wa mifumo sahihi ya uendeshaji wa skimu ndogo, za kati na kubwa;

(viii) Kuhamasisha matumizi ya umwagiliaji kwa mazao mbalimbali na kwa misimu zaidi ya mmoja.;

(ix) Kuwezesha wakulima wamwagiliaji katika upatikanaji wa huduma za zana za kilimo, pembejeo na huduma za ugani kwa ajili ya uzalishaji mazao wenye tija;

(x) Kuwezesha wamwagiliaji katika upatikanaji wa teknolojia mbalimbali za kuongeza mnyororo wa thamani ya mazao ili kupata soko zuri lenye kuleta tija.

(xi) Kutoa mchango muhimu katika uandaaji wa sera na mikakati ya kuendeleza umwagiliaji na matupio.

Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi na itakuwa na sehemu mbili zifuatazo:

(i) Sehemu ya Huduma za Uendeshajina

(ii) Sehemu ya Huduma za Usaidizi.

1.1 Sehemu ya Huduma za Uendeshaji

Sehemu hii itatekeleza shughuli zifuatazo:-

(i) Kuhamashisha matumizi ya teknolojia sahihi katika kilimo cha umwagiliaji;

(ii) Kuhamasisha matumizi bora ya maji na agronomia katika kilimo cha umwagiliaji;

(iii) Kuhakikisha kuwa kiasi cha maji yanyopelekwa shambani kinalingana na kibali cha matumizi ya maji kilichotolewa;

(iv) Kutunza na kuhakiki taarifa za uzalishaji mazao kwa ajili ya kubaini mchango wa umwagiliaji kwenye usalama wa chakula;

(v) Kuwezesha uandaaji wa mipango ya uendeshaji na matengenezo ya skimu za umwagiliaji katika kila mwisho wa msimu na kufanya matengenezo ya mfumo wa umwagiliaji;

(vi) Kuwezesha uandaaji na usimamizi wa ratiba za matumizi bora ya maji shambani;

(vii) Kuwezesha ukusanyaji na matumizi bora ya ada za huduma za umwagiliaji na ada nyinginezo;

(viii) Kuhamasisha matumizi ya umwagiliaji kwa mazao mbalimbali na kwa misimu zaidi ya mmoja.

Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.

3.4.2 Sehemu ya Huduma za Usaidizi

Sehemu hii itatekeleza shughuli zifuatazo:-

(i) Kuandaa na kusambaza miongozo ya usimamizi wa vyama vya wamwagiliaji;

(ii) Kusaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa kuunda Timu za Wataalamu za kusimamia uendeshaji wa skimu za umwagiliaji;

(iii) Kusaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa na Vyama vya Wamwagiliaji katika kuandaa na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogokwa mujibu wa Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji na kanuni zake;

(iv) Kusaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa kuanzisha na kutunza takwimu za umwagiliaji na kuziunganisha na takwimu za kitaifa;

(v) Kuwezesha uanzishwaji wa mifumo sahihi ya uendeshaji wa skimu ndogo, za kati na kubwa;

(vi) Kuwezesha wamwagiliaji katika upatikanaji wa teknolojia mbalimbali za kuongeza mnyororo wa thamani ya mazao ili kupata soko zuri lenye kuleta tija

(ix) Kuwezesha uanzishaji na uimarishaji wa vyama vya wamwagiliaji;

Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.