Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini

Madhumuni

Kutoa utaalamu na huduma katika mipango, bajeti, ufuatiliaji na tathmini.

Idara hii itafanya kazi zifuatazo:-

(i) Kuratibu utayarishaji na utekelezaji wa mipango na bajeti ya Tume;

(ii) Kuhamasisha na kuwezesha utoaji huduma kwa sekta binafsi;

(iii) Kutayarisha mchango wa ofisi katika taarifa ya bajeti na taarifa ya kiuchumi ya mwaka;

(iv) Kuweka mfumo wa utayarishaji wa mpango mkakati na kwa kuzingatia ujuzi wa kuandaa bajeti ya Tume;

(v) Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa sera za Serikali;

(vi) Kufanya uchambuzi wa sera za sekta mbalimbali na kutoa ushauri stahiki;

(vii) Kufanya ufuatiliaji na tathmini katika mipango na bajeti ya Tume na kutayarisha taarifa za utekelezaji;

(viii) Kutafiti, kuchambua na kufanya tathmini ya mipango kwa ajili ya kutoa maamuzi ya mwelekeo wa baadae wa Tume;

(ix) Kuhakikisha kwamba mipango na bajeti ya Tume inajumuishwa katika taratibu za bajeti ya Serikali; na

(x) Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa miradi / mipango ya maendeleo na upatikanaji wa rasilimali.

Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi na itakuwa na vitengoviwili kama ifuatavyo:

(i) Kitengo cha mipango; na

(ii) Kitengo cha Ufuatiliaji naTathmini.

1.1 Kitengo chaMipango

Kitengo hiki kitafanya kazi zifuatazo:-

(i) Kuratibu uandaaji na utayarishaji wa mpango wa mwaka na mpango mkakati wa muda wa kati;

(ii) Kuweka pamoja miradi, mipango, mipango kazi na kuweka mikakati ya upatikanaji wa rasilimali;

(iii) Kuwasiliana na Wizara ya Fedha na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma juu ya michakato ya mipango mkakati na bajeti;

(iv) Kutoa miongozo ya kitaalamu na kusaidia uwepo wa mpango mkakati na bajeti;

(v) Kushiriki katika uchambuzi wa kazi zisizo za msingi zinazoweza kufanywa na sekta binafsi; na

(vi) Kutayarisha mkataba wa makubaliano kwa miradi na program yenye ufadhili wa kimataifa;

Kitengo hiki kitaongozwa na Mchumi Mkuu

1.2 Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini

Kitengo hiki kitafanya kazi zifuatazo:-

(i) Kufuatilia utekelezaji wa mpango wa mwaka wa Tume pamoja na mpango mkakati wa muda wa kati;

(ii) Kutayarisha taarifa za utekelezaji wa mpango kwa vipindi maalumu (juma, mwezi, robo mwaka, nusu mwaka na mwaka);

(iii) Kukusanya na kuchambua takwimu zinazohitajika katika utayarishaji na utekelezaji wa sera, mipango na mapendekezo ya bajeti;

(iv) Kutoa mchango katika utayarishaji na uaandaji wa mipango na bajeti za Tume ikiwa ni pamoja na kuweka malengo muhimu na viashiria;

(v) Kutoa usaidizi wa kitaalamu ikiwa ni pamoja na kuweka mfumo wa ufuatiliaji na tathmini;

(vi) Kufanya utafiti wa matokeo ya mipango, miradi na programu mbalimbali;

(vii) Kufanya tathmini ya hali ya utoaji huduma kwa kukusanya maoni ya wadau juu ya huduma zinazotolewa; na

(viii) Kuratibu mapitio ya utekelezaji wa mipango ya nusu mwaka na ya mwaka.

Kitengo hikikitaongozwa na Mchumi Mkuu