Habari
TUME YATAKIWA JENGA MFUMO WA KUSIMAMIA SKIMU ZA UMWAGILIAJI NCHINI.

Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Hussein Bashe ameitaka Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kujenga mfumo imara wa kusimamia Skimu za Umwagiliaji nchini na kusisitiza kuwa kipaombele cha Wizara yake katika Mwaka wa fedha 2022- 2023 ni Umwagiliaji.
Akizungumza katika kikao kazi na Menejimenti hiyo jijini Dodoma, Mheshimiwa Bashe ametaja vipaumbele vingine kuwa ni pamoja na kuandaa mfumo wa kibiashara utakao weza kuzalisha faida inayotokana na uwekezaji wa miradi mbalimbali inayowekezwa na Tume.
Mheshimiwa Bashe amesema Tume ihakikishe asilimia 50% ya bidhaa zitokanazo na mazao zinazalishwa nchini kupitia kilimo cha Umwagiliji ifikapo mwaka 2030 ambapo ameitaka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kujenga miradi mikubwa ya kimkakati ya Umwagiliaji.
“Nataka Tume hii ifanye miradi ya Umwagiliaji kama tunavyo zindua miradi ya SGR, kama tunavyozindua miradi ya Stigler, tunahitaji miradi kama Stiglers kwenye Umwagiliaji”
Mheshimiwa Bashe pia amesisitiza Menejimenti pamoja na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kufanya kazi kwa bidii, weledi, ikiwemo muda wa ziada ili kufanikisha malengo yaliyowekwa na Serikali kufikia Hekta Milioni Moja lakimbili (1,200,000) Mwaka 2025.
GCU