Habari

UJENZI WA BWAWA LA MSAGALI MPWAPWA DODOMA WAFIKIA 16%

UJENZI WA BWAWA LA MSAGALI MPWAPWA DODOMA WAFIKIA 16%
Feb, 07 2023

Ujenzi wa Bwawa la Msagali Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma umefikia zaidi ya asilimia 16, ujenzi wa Bwawa hilo unatekelezwa na mkandarasi MS/GNMS Contractors Co. Ltd.

Lori likijaza udongo katika eneo la ujenzi

 

Bwawa la Msagali linarajiwa kuwa na ujazo wa mita za ujazo milioni 92, maji ya Bwawa hili yatatumika kwa shughuli za umwagiliaji, mifugo na masuala mengine ya kijamii.

Vijiji vitakavyonufaika na mradi huu ni Ng’ambi na Msagali.

Mradi wa Bwawa la Msagali utaongeza ajira na kuinua uchumi wa wakazi wa Mpwawa kupitia kilimo cha umwagiliaji ambapo wakulima watalima mara 2 au 3 kwa mwaka kutegemea na aina ya mazao.

Greda likisambaza kifusi katika eneo la ujenzi.