Habari

MKURUGENZI MKUU WA TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI AWASA WAFANYAKAZI KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO NA KUZINGATIA WELEDI NA UZALENDO

MKURUGENZI MKUU WA TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI AWASA WAFANYAKAZI KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO NA KUZINGATIA WELEDI NA UZALENDO
Jun, 24 2023

Mkurugenzi mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji NIRC Bw. Raymond Mndolwa amewaasa
wafanyakazi wa Tume kufanya kazi kwa ushirikiano na kuongeza bidii kwa kuzingatia weledi na
uzalendo na kuweka mbele maslahi ya taifa ili kuchochea maendeleo ya nchi katika sekta ya
kilimo cha umwagiliaji.
Bw. Mndolwa ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano na wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya Tume jijini Dodoma amesema
ushirikiano baina ya wafanyakazi ni matokeo chanya katika kuunga mkono juhudi za serikali
inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo katika sekta ya kilimo.
"Tunatakiwa tuwe na mawasiliano, tuambizane turekebishane, tushirikishane, kanuni yangu
mimi vitu vyote ntaweka juu ya meza nawaita wenzangu tunashauriana, tunakubaliana, twendeni
na taratibu hizo za kushirikishana" alisema Mndolwa.
Aidha Mndolwa amewaasa watumishi hao kutumia vizuri rasilimali za serikali kwa maslahi ya
taifa badala ya kutumia rasilimali hizo kwa matumizi binafsi ikiwemo magari ya Tume pamoja
vifaa vingine vinavyotumika kurahisisha shughuli za taasisi.
Hata hivyo Mndolwa amesema katika kuboresha shughuli za ukusanyaji ada za huduma za
umwagiliaji katika skimu zote nchini Tume imejipanga kununua magari katika kila skimu ili
kurahisisha zoezi la utoaji elimu ya ada za huduma za umwagiliaji pamoja na ukusanyaji ada
hizo kwa wakulima.
"Tunanunua magari ya skimu kila skimu itakuwa na gari na tutakuwa na maofisa wa skimu ili
waweze kukusanya ada za huduma za umwagiliaji"
Aidha awali kabla ya mkutano huo Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw.
Raymond Mndolwa alifanya kikao na Wahandisi wa Mikoa kwa njia ya mtandao ambapo
amewataka wahandisi hao pamoja na watumishi wa tume mikoa kuongeza kasi katika zoezi la
ukusanyaji ada za huduma za umwagiliaji.
02 JUNE 2023