Habari

TUME YATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI BASHE, UKARABATI KITUO CHA VIJANA BIHAWANA WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 90%.

TUME YATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI BASHE, UKARABATI KITUO CHA VIJANA BIHAWANA WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 90%.
Feb, 08 2023

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji mbioni kukamilisha ukarabati wa kituo cha mafunzo ya kilimo kwa vijana katika eneo la BIHAWANA nje kidogo ya jiji la Dodoma.  

Jengo la utawala.


Shughuli zilizotekelezwa na Tume ni pamoja na ukarabati wa miundombinu ya kijamii kamavile mabweni, ukumbi wa kulia chakula, kupumzikia, njia za miguu na vyoo.
Kwasasa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ina malizia kukarabati miundombinu ya mifereji katika barabara kuu ya kuingilia mashambani ili kudhibiti mmomonyoko wa udongo unaoweza kuharibu barabara wakati wa mvua.

Muonekano wa Bweni baada ya kufanyiwa ukarabati.


Zoezi la kusawazisha eneo la shamba pia inaendelea kwa hatua mbalimbali.
Program ya BBT – YIA ilizinduliwa na Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa tarehe 3 mwezi wa 8  katika maadhimisho ya siku ya wakulima nane nane mkoani Mbeya.
Program hii inalenga kuwafikia vijana elfu tatu na kuongeza ukuaji wa sekta ya kilimo kufikia asilimia 10 mwaka 2030 (agenda 10/30)

Mafundi wakimalizia kukarabati njia za kuingia Bwenini.

 

Matayarisho ya shamba la kufundishia.

 

 Mafundi wakijenga miundombinu ya mfereji katika barabara kuu ya shamba darasa.

 

Vitalu nyumba kwaajili ya kufundishia. 

 

Mfumo wa Umeme jua katika shamba darasa la Bihawana.