Habari

TEKNOLOJIA YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI INAYOWEZA KUMSAIDIA MKULIMA KUINGIA KATIKA KILIMO BIASHARA NZUGUNI - DODOMA

TEKNOLOJIA YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI INAYOWEZA KUMSAIDIA MKULIMA KUINGIA KATIKA KILIMO BIASHARA NZUGUNI - DODOMA
Aug, 05 2022

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imekuja na Teknolojia mbali mbali zitakazoweza kumsaidia mkulima katika kilimo cha umwagiliaji ili kupunguza gharama za uzalishaji, na  ziweze kumuongezea kipato yani kilimo biashara katika maonesho ya kilimo ya kikanda jijini Dodoma.

Akiongea katika viwanja yanapofanyika maonesho hayo kikanda Nzuguni  mkoani Dodoma, Mhandisi Raphael Laiza amesema, “Kwenye banda letu hapa Dodoma, tumekuja na teknolojia ya kutumia mfumo wa umeme wa jua , wa kuchimba maji chini na kujenga kisima na kuhifadhi maji kwa ajili ya kilimo, mifumo hii ni rahisi na kuna mazao ya mfano ambayo yameyapanda na yamefanya vizuri tena ni mazao ya biashara ambapo mkulima anaweza kutumia na kupata faida.” Alisema Mhandisi

Mhadisi Laiza alisema teknolojia nyingine zinazotumika katika kilimo cha umwagiliaji zinatofautina katika ufanisi kama vile, teknolijia ya matone yaani drip irrigation yenye ufanisi wa 90%, surface irrigation yenye ufanisi wa 40%, spinklers yaaani njia ya mvua yenye ufanisi wa 50%.

Aliongeza kwa kusema kuwa, mkoa wa Dodoma upatikanaji wa vyanzo vingi vya maji ni vigumu na vinapatikana kwa shida na maeneo mengi hayana vyanzo vya kudumu na maeneo mengi ya Dodoma hayana mito ya kudumu yanategemea mito ya misimu, “kwa Mwaka huu wa fedha 2022 -2023 katika mkoa huu wa Dodoma tumepanga kujenga mabwawa ikiwa ni pamoja na msagawa na membe.” Alisisitiza

Teknolojia hii itasaida sana kupunguza gharama za maji kwa mkulima hasa katika mkoa wa Dodoma.

Maonesho haya ya wakulima kitaifa mwaka huu yanafanyika Mkoani Mbeya.