Habari

Kilimo cha mpunga kilombero kuwakomboa watanzania

Kilimo cha mpunga kilombero kuwakomboa watanzania
Jun, 06 2018

Zao hili linaloshamiri kwa haraka na kuongeza heshima kwa Mkoa wa Morogoro kama ghala la chakula, ni pamoja na mpunga ambao kwa siku za karibuni limeongeza umaarufu miongoni mwa mazao ya chakula na biashara yanayoingiza kipato kwa wakulima nchini na kutegemewa na wananchi wa Wilaya ya Kilombero katika kukuza uchumi.soma zaidi

Hata hivyo, kilimo cha mpunga kwa nchi zinazoendelea kinakabiliwa na changamoto nyingi zinazokwamisha maendeleo ya uzalishaji wake na kubwa ikiwa ni kutegemea mvua kama chanzo kikuu cha maji kwenye kilimo cha mpunga kwa wakulima wadogo.

Viwango vya mahitaji ya maji katika kukua kwa mpunga hutofautiana miongoni mwa aina za mpunga na maeneo ya uzalishaji kutoka wilaya moja hadi nyingine.

Ni kwa jinsi hii mpunga hupandwa katika mazingira mbalimbali kwa kutegemea mahitaji yake ya maji.

Wataalamu wameshabainisha aina tatu kuu za mazingira yanayolimwa mpunga kulingana na upatikanaji wa maji na hali ya mwinuko wa nchi. Mazingira haya ni kilimo cha mpunga wa mabondeni kinachotegemea mvua kwa asilimia 72, kilimo cha mpunga wa kwenye miinuko (20%) na kilimo cha mpunga cha umwagiliaji (8%).

Maeneo yanayolima mpunga kwa wingi Tanzania ni Morogoro maeneo ya Bonde la Kilombero/Ifakara, Dakawa, Malolo, Mbeya, Kyela, Mbarali, Shinyanga, Kahama, Mwanza, Magu, Geita na Sengerema, Bonde la Ruvu mkoani Pwani na Bonde la Mto Rufiji na mengineyo.soma zaidi