Habari
UJENZI BWAWA LA MEMBE WAFIKIA 45.83%

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Rosemary Senyamule ameitaka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kusimamia kwa makini ujenzi wa Bwawa la Membe linalojengwa Wilayani Chamwino na kuhakikisha kuwa bwawa hilo linakidhi vigezo vinavyotakiwa ili lidumu kwa muda mrefu.
Akizungumza na baadhi ya wanavijiji watakao nufaika na Bwawa hilo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa bwawa katika eneo la mradi, mkuu huyo wa Mkoa amewaeleza wananchi wa Membe hatua madhubuti zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha Wilaya ya Chamwino na mkoa wa Dodoma kwa ujumla unaondokana na tatizo la njaa kupitia kilimo cha umwagiliaji ambacho ni cha uhakika.
Bwawa la Membe linatarajiwa kuwa na mita za ujazo wa Milioni 12, maji ya Bwawa hili yatatutumika kwa shughuli za umwagiliaji, mifugo na masuala mengine ya kijamii.

Vijiji vitakavyonufaika na Bwawa hilo ni Membe, Chitabuli, Mlimwa, Dabalo pamoja na wakazi wa Tarafa ya Chilonwa.
Mradi wa Bwawa la Membe utaongeza ajira katika kilimo na kuinua uchumi kwa wakazi wa Mpwawa kupitia kilimo cha umwagiliaji ambapo wakulima watalima mara 2 au 3 kwa mwaka kutegemea na aina ya mazao.
Gharama za ujenzi ni Bilioni 12 na muda wa ujenzi ni miezi 12.

