Habari

TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI NIRC YATUNUKIWA CHETI CHA PONGEZI KWA KUWA NA MKATABA HUDUMA KWA MTEJA.

TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI NIRC YATUNUKIWA CHETI CHA PONGEZI KWA KUWA NA MKATABA HUDUMA KWA MTEJA.
Jun, 24 2023


Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene (Mb) ameitunuku Tume ya Taifa ya Umwagiliaji NIRC cheti cha pongezi kwa kuwa na mkataba wa huduma kwa mteja.
Waziri Simbachawene ametoa cheti hicho wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mikataba ya Huduma kwa Mteja kwa Taasisi za Umma iliyofanyika jijini Tanga, ambapo mewaasa watumishi wa umma kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kutoa huduma bora kwa wateja na kuweka kando maslahi binafsi.
Akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu  Bi. Maria Itembe amewataka watumishi wa Tume kuusoma mkataba huo, kwa kuwa ndio nyenzo yenye mwongonzo wa utoaji huduma kwa wananchi ambao ndio wateja.
Hata hivyo Waziri Simbachawene ameitunuku Wizara ya Kilimo tuzo maalum kwa kuhamasisha taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kuandaa mkataba wa huduma kwa mteja.
Mkataba wa huduma kwa mteja unalenga kumsaidia mteja kuifahamu Tume pamoja na huduma zinazotolewa ikiwemo  kuimarisha mahusiano mazuri kati ya Tume na wateja wake na hivyo kupunguza malalamiko katika utoaji wa huduma.
 Aidha Mkataba huo unatoa nafasi kwa mteja kuwa huru kutoa maoni ya namna bora ya kuboresha huduma zake kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa na utaongeza uwajibikaji kwa watumishi wa Tume kwa kutekeleza dhana ya uwajibikaji kwa vitendo.