Habari

NIRC IMEDHAMIRIA KUJENGA UZIO KATIKA SKIMU ZA UMWAGILIAJI KUZUIA UTOROSHAJI MAZAO NA WANYAMAPORI WANAOHARIBU MAZAO.

NIRC IMEDHAMIRIA KUJENGA UZIO KATIKA SKIMU ZA UMWAGILIAJI KUZUIA UTOROSHAJI MAZAO NA WANYAMAPORI WANAOHARIBU MAZAO.
Jun, 24 2023

Mkurugenzi mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) Bw. Raymond Mndolwa amewataka wakulima wanaolima katika skimu za  umwagiliaji nchini kulipia ada ya huduma ya umwagiliaji iliyowekwa kwa mujibu wa sheria  ili kuwezesha ukarabati, ujenzi na uwekezaji katika  Miundombinu ya Umwagiliaji Kwa lengo la kukuza sekta ya Kilimo Cha  Umwagiliaji Nchini.
Mndolwa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wakulima wa Chama cha Ushirika Ruvu CHAURU wilayani  Bagamoyo mkoani Pwani ambapo amesema Tume imedhamiria kujenga uzio katika Skimu za Umwagiliaji kwa lengo la kuzuia utoroshaji wa mazao Kwa wakulima wenye tabia ya kukwepa kulipa Ada ya Umwagiliaji Iakini pia kuzuia wanyama pori wanaoharibu mazao ya wakulima.
Amesema ni jukumu la Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ni kujenga miundombinu ya umwagiliaji pamoja na jukumu la kukusanya ada za huduma za umwagiliaji.
"Kwa kuwa serikali haitoi fedha za kurekebisha miundombinu ya umwagiliaji tuna wajibu sisi kama wakulima kurudisha kidogo kwenye sehemu ile ambayo sisi tumepata, wakulima wanakuwa wazito kuchangia hilo kwa sababu ya kutofahamu ndilo limenifanya nije hapa" Amesema Mndolwa.
 Kwa upande wao baadhi wakulima hao wameeleza manufaa watakayopata kutokana na uchangiaji Huduma za Umwagiliaji ikiwa ni pamoja na ukarabati wa miundombinu chakavu pamoja na kudhibiti upotevu wa maji.
Aidha Mndolwa amesema katika kuboresha zoezi la ukusanyaji ada hizo Tume ipo mbioni kununua vishikwambi vitakavyotumiwa na wataalam wa Tume wakati wa zoezi la ukusanyaji Ada ya Umwagiliaji ili kupata taarifa za sahihi za zoezi hilo.
08 JUNE 2023