Habari

NIRC KUTUMIA SHILINGI BILIONI MBILI KWA AJILI YA UKARABATI WA MITAMBO

NIRC KUTUMIA SHILINGI BILIONI MBILI KWA AJILI YA UKARABATI WA MITAMBO
Jan, 27 2022

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw, Daudi Kaali amesema, Tume imeandaa bajeti ya Shilingi Bilioni Mbili kwaajili ya ukarabati wa Mitambo yake yote.

Bw. Kaali amesema Tume ina jumla ya Mitambo 53 na inayoweza kutengenezwa ni Mitambo 44 na malengo yaliyowekwa na Tumeni kutengeneza mitambo 43 hadi kufikia mwakani 2023. “Tutaokoa fedha nyingi kwani kukodi Mtambo mmoja siyo chini ya Sh. Milioni moja kwa siku moja na unaweza kukuta, Skimu moja inaweza ikahitaji siku hata ishirini au thelathini kwa ajili ya matengenezo , hivyo kwa mahesabu ya haraka utaona ni fedha nyingi sana zinahitaji kukodisha mtambo mmoja kwa siku”. Alisisitiza Kaali.