Habari
Prof. Mahoo amtaka Mkandarasi kurekebisha kasoro Bwawa la Endagaw
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Prof, Henry Mahoo amemtaka Mkandarasi waKampuni ya GOPA Contractors kurekebisha kasoro alizobaini wakati wa kukagua ujenzi wa tuta la Bwawa la kuhifadhi maji yanayotumika kwa shughuli za Umwagiliaji katika Skimu ya Endagaw iliyoko Wilayani Hanang Mkoani Manyara.
Akizungumza katika eneo hilo, Prof, Mahoo amemshauri Mkandarasi GOPA Contractors kuziba maeneo yanayovujisha maji katika Bwawa hilo vinginevyo Tume ya Taifa ya Umwagiliaji haitakuwa tayari kuupokea mradi huo.