Habari

Mkandarasi, Meneja, Meneja, kamati ya Ujenzi Kirya kuainisha maeneo ya kijamii.

Mkandarasi, Meneja, Meneja, kamati ya Ujenzi Kirya kuainisha maeneo ya kijamii.
Feb, 15 2022

Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji miundombinu Mhandisi, Kimasa Ntonda amewataka Mkandarasi kwa kushirikiana na Meneja wa Mradi pamoja na kamati ya Ujenzi kuoanisha maeneo yanayohitaji kufanyiwa maboresho ili maamuzi yafanyike kupitia bajati iliyopo kwakuwa mradi huo una ukomo wa matumizi ya fedha zilizopangwa kutumika kwa shughuli ya ujenzi.

Aidha Mwenyekiti wa Bodi ya Tume Prof, Henry Mahoo, amewashauri wadau wote wanaousika katika mradi huo kuendelea kushirikiana kwa pamoja ili kufanikisha ujenzi wa mradi huo.

Ujenzi wa Miundombinu katika Skimu ya Kiryaumefikia asilimia 30%

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeingia mkataba wa ujenzi wa Miundombinu Skimu ya Kirya na kampuni ya JV kwa ubia na kampuni ya ujenzi ya PETRA wenye thamani ya shilingi Bilioni mmoja za kitanzania.(1,000,000,000/=)