Habari

Tangazeni mafanikio ya Serikali - Majaliwa awaambia Maafisa Habari

Tangazeni mafanikio ya Serikali - Majaliwa  awaambia Maafisa Habari
Mar, 26 2019

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano Serikalini kutangaza kwa kina mafanikiona mageuzi makubwa yanayofanywa naserikali ili umma wa Watanzania uweze kujuakwani hiyoni haki yao ya kikatiba.

Waziri Mkuu aliyasema hayo hivi karibuni katika ufunguzi wa Kikao Kazi cha 15 cha Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano Serikalini, kilichofanyika katika ukumbi wa BOT jijini Mwanza. Kikao hicho kilihudhuriwa na Maafisa Habari takbaribani 400.

Mhe. Majaliwa amewataka Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano Serikalini kutumia njia anuwai na bora za kuyatangaza na kuyatetea mafanikio ya serikali.

Ameongeza kuwa Maafisa Habari nchini wahakikishe wanatumia vizuri taaluma zao na nyezo wanazopatiwa kutangaza mambo yanayofanywa na serikali kwenye sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, elimu, afya nishati; mifugo; viwanda,uchukuzi, madini, utalii, sanaa za filamuna michezo.

Waziri Mkuu amewaasa Maafisa Habari hao kuwa wasipotangaza mafanikio ya serkali kwa kina na ufasahawatatoa fursa kwa taarifa zinazosemwa na wapinga maendeleo kuonekana kuwa ni kweli.

“Utoaji taarifa kwa wananchi kwa sasa si utashi binafsi wa mtoa habari bali ni kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi” Alisema, Majaliwa na kuongeza kuwa mathalan Sheria mpya ya Haki ya Kupata Taarifa Na. 12 ya mwaka 2016 yenye kuzitaka mamlaka za umma kuwapa wananchi taarifa zinazowahusu.

Aidha Waziri Mkuu amewataka viongozi na watendaji wa Wizara, taasisi za umma na Halmashauri zote nchini kuwashirikisha maafisa Habari wao katika vikao vyote vya maamuzi na shughuli mbalimbali zinazofanywa katika maeneo yao kwani wao ni daraja la kutoa taarifa kati ya serikali nawananchi.