Habari

MKANDARASI AKABIDHIWA ENEO LA UJENZI WA BWAWA LENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI KUMI NA MOJA CHAMWINO.

MKANDARASI AKABIDHIWA ENEO LA UJENZI WA BWAWA LENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI KUMI NA MOJA CHAMWINO.
Sep, 01 2022

Ujenzi kukamilika ndani ya mwaka mmoja.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amemtaka mkandarasi NAKUROI CONSTRACTORS, kukamilisha ujenzi wa Bwawa litakalotumika kwa kilimo cha Umwagiliaji lililopo Membe wilayani Chamwino kwa wakati uliopangwa baada ya kukabiziwa eneo la ujenzi wa mradi huo.

Picha 1

Mhe. Senyamule, Serikali imedhamiria kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo ili kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na uchumi wananchi kwa ujumla. “Mkandarasi anatakiwa kujenga mradi huu kwa mwaka mmoja  hivyo tunawaomba wananchi wa hapa membe kuwa wasimamizi wa huu mradi, ni wakwenu na muwe walinzi  maana fedha zinazojenga mradi huu ni za kwenu.” Alisisitiza mkuu wa Mkoa.

Picha 2

Akiongea wakati wa kukabidhi mradi huo kwa Mkandarasi, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Gift Msuya amempongeza Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe kwa kuwa na utashi wa kuhakikisha kwamba mambo makubwa ambayo Mhe Rais anatarajia yatokee katika sekta ya kilimo yanafanikiwa kwa kiasi kikubwa na kwa viwango vya hali ya juu. “Sisi wenyewe tumekuwa mashahidi wa mambo makubwa na mapinduzi makubwa yanayokwenda kutokea katika wizara hii ya kilimo.” Alisema

Kwa upande wake Mhandisi wa Umwagiliaji wa Wilaya ya Chamwino Salehe Madebe amesema, bwawa hilo litakuwa na ujazo wa Cubic metres Milioni 5.1. Tumeweza kuweka mikakati ya kujenga bwawa hili ambalo litadumu kwa muda mrefu, bwawa ambalo litakidhi mahitaji ya kilimo cha umwagiliaji ambapo itajengwa skimu yenye ekari elfu nane, malambo ya kunyweshea mifugo na matumizi ya nyumbani.

Picha 3

“Naomba viongozi katika ngazi zote tushirikiane kwa pamoja kuhakikisha mradi huu unatekelezwa kwa wakati.” Alifafanua.

Mradi wa Bwawa la Membe ni moja kati ya miradi 21 ya kilimo cha Umwagiliaji iliyosainiwa mbele ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya sikukuu ya wakulima nanenane yaliyofanyika kitaifa mkoani Mbeya mwaka huu.