Habari

ONGEZOKO BAJETI SEKTA YA UMWAGILIAJI ASILIMIA 100

ONGEZOKO BAJETI SEKTA YA UMWAGILIAJI ASILIMIA 100
Mar, 24 2022

Mwenyekiti wa bodi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Profesa Henry Mahoo ameishukuru Serikali kwa kuongeza fedha za Maendeleo katika Sekta ya Kilimo cha Umwagiliaji kutoka Shilingi Bilioni 46.5 hadi Shilingi Bilioni 146.5 ongezeko la asilimia mia moja kwa mwaka wa fedha 2022/2023 hatua itakayoharakisha mapinduzi ya kilimo cha Umwagiliaji na kuongeza tija katika uzalishaji.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali, amesema kuwa Tume inashirikiana na sekta Binafsi katika kuendeleza mikakati ya pamoja kutumia fursa zilizopo katika sekta binafsi ili ziweze kuchangia katika uendelezaji wa kilimo cha umwagiliaji nchini.