Habari
Uzalishaji wa mpunga Mbeya waongezeka
Uzalishaji wa mpunga Mbeya waongezeka
Na Mwandishi Wetu, Mbeya
UZALISHAJI wa zao la mpunga mkoani Mbeya umekuwa ukiongezeka kwa wastaniwa tija katika kipindi cha miaka minne kuanziamwaka 2016/2017 ambapo uzalishaji ulikuwa tani 2.8 kwa hekta, mwaka 2017/18 ulikuwa tani 3.1 kwa hekta na mwaka 2018/2019 uzalishaji ulikuwa tani 4.63 wa hekta.
Hayo yameelezwa jana na Afisa Kilimo wa Umwagiliaji wa Mkoa wa Mbeya Bwn. Wilfred Kayombo alipotembelewa ofisini kwakena Wataalamu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
Bwana Kayombo ameeleza kuwa katika mwaka wa 2019/2020 mkoa wa Mbeyanatarajia kuwa na ongezeko la zaidi ya wastani wa tija hadi kufikia tani 5.0 kwa hekta
kutokana na matumizi ya mbegu bora, pembejeo na teknolojia za kisasa za umwagiliaji.
Aidha,Mhandisi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mkoa wa Mbeya Elibariki Mwendo amesema kuwa kutokana na matumizi ya mbegu bora na teknolojia ya kisasa tofauti na zamani uzalishaji wa mpunga umeongezeka hususan katika Wilaya za Mbarali, Kyela,Busokelo na Mbeya Vijijini ambapo wakulima wengi hutumia mbegu bora ikiwemo aina ya SARO.
Akielezea hali ya uzalishaji wa kilimo cha umwagiliaji katika Wilaya ya Mbarali Mhandisi Mwendo amesema kwa zao la mpunga uzalishaji umeongezeka kutoka tani 3 hadi 5.4 kwa hekta, mahindini tani 2.3 hadi 3,5 kwahekta, vitunguu ni tani 10 hadi 11 kwa hekta wakati nyanya ni tani 21 hadi 40 kwa hekta.
Bwana Mwendo amesema kilimo cha umwagiliaji mkoani Mbeya kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uharibifu wa mazingira katika sehemu za miinuko unaosababisha maji kusafirisha udongo na mchanga mwingi maeneo ya mabondeni jambo linalosababisha mito kufurika, kujaa mchanga hata kubadili mwelekeona hatimayeuharibifu wa miundombinu ya umwagiliaji, ongezeko la watu wanaotegemea kilimo cha umwagiliaji katika bonde la Ruaha Mkuu inazidi kuongezeka hivyo kupanua maeneo zaidi wakati maji yakizidi kupungua.
Aidha, Mhandisi Mwendo amesema, changamoto nyingine ni matumizi mabaya ya maji katika Kilimo cha Umwagiliaji kwa wakulima wadogo wadogo hususan katika skimu za asili ni ya ufanisi wa chini kutokana na elimu ndogo ya wakulima.
Katika kutatua changamoto hizo Mhandisi Mwendo amesema Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeandaa Mkakati Kabambe wa Umwagiliaji wa Mwaka 2018 (National Irrigation Master Plan) wa kuanzia mwaka 2020 - 2035 kwa ajili ya kuboresha Skimu za Umwagiliaji zote nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Mabwawa kwa ajili ya kilimo cha Umwagiliaji na matumizi mengine, Kuhamasisha wananchi kutunza mazingira ili rasilimali maji kuwa endelevu.
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na ikisaidiana na Halmashauri mbalimbal za Wilaya kuendelea kutafuta fedha kutoka kwenye vyanzo mbalimbali kwa ajili ya kuendelea kujenga miundombinu kwenye Skimu za Umwagiliaji kwa lengo la kuongeza Uzalishaji wa Mazao ya chakula, matunda na mbogamboga ikiwa ni pamoja ufanisi wa matumizi bora ya rasilimali za maji kwa kufuata sharia, uwepo wa Mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kupunguza migogoro.
Tume ya Taifa ya Umwagiliajiinaendelea kutoa elimu kwa wakulima wadogo wadogo juu ya matumizi bora ya maji, utunzaji bora wa mimea na matumizi teknolojia ya kilimo cha mpunga kwa kutumia maji kidogo.
Aidha Mhandisi Mwendo amesema kuwa kutokana na kuwepo kwamiradi mingi ya umwagiliaji inayohitaji fedha, wakulima wanashauriwa kukopa fedha kutoka taasisi mbalimbali za kifedha kwa ajili ya kuendeleza na kuboresha miundombinu ya umwagiliaji kwenye skimu zao kwa kushirikiana na wataalamu wa umwagiliaji waliopo Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na Halmashauri husika.
MWISHO.