Habari

Wakulima Mbulu Waiomba Serikali Kuwaleta Wataalam wa Kilimo

Wakulima Mbulu Waiomba Serikali Kuwaleta Wataalam wa Kilimo
Jun, 30 2019

Wakulima Wilayani Mbulu wameiomba serikali iwapelekee wataalamu wa kilimo na pembejeo za kutosha ili kuwawezesha kuwa na kilimo chenye tija zaidi.

Ombi hilo lilitolewa na umoja wa Wamwagiliaji wa Skimu ya umwagiliaji ya Mangisa iliyopo katika kata ya Dongpbeshi, Wilayani Mbulu Mkoani Manyara walipokuwa wakiongea na waandishi wa habari na wataalamu kutoka Tume ya Taifa yaUmwagiliaji jana walipoitembelea skimu hiyo.

Akizungumza kwaniaba ya umoja wa Wamwagiliajikatibu wa umoja huo Damiano Sulle alisema serikali kwa kushirikiana na wafadhili ilifanya jambo la msingi kuleta skimu ya umwagiliaji katika eneo hiloambapo ameeleza kuwa imeleta tija kwani ndio ajira pekee iliyo badilisha maisha ya wakazi wengi katika kata ya Dongobeshii.

“Kabla ya kuwepo kwa skimu hii mkulima aliweza kuvuna chini ya gunia kumi (10) kwa tani au kumi na tano (15) za kitunguu saumu kwa hekta na baada ya kuboreshwa kwa miundombiu ya kisasa ya umwagiliaji mkulima anaweza kupata hata gunia hamsini (50) ya zao hio kwa hekta” Alisema Bwana Sulle.

Sulle ameiomba serikali kuwasaidia kusakafia mfereji ambao haujasakafiwa wenye urefu wa mita 50 ambao utawasaidia wakulima kujipanga vizuri hasa katika matumizi sahihi ya maji na kuongeza uzalishaji zaidi wa mazao.

Sambamba na hilo wakulima wameomba serikali kuwatafutia soko la uhakika hususan la zao la kitunguu swaumu ili waweze kuuza zao hilo kwa mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani kwani wana maghala makubwa ya kutosha ambapo wangeweza kuhifadhi mazao hayo na kuuyauza wakati ambao bei za mazao hayo zikiwa juu.

Wilaya hiyo ya Mbulu ina eneo la Hekta 2400 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji na hekta 1250 ndizo zinazotumika kwa kilimo hicho ambapo kuna skimu saba ambazo ni Mangisa, Dongobeshi, Tumati, Diyomati, Dirm, Ari na Bashay skimu ambazo zinatumika kwa kilimo cha zao la mahindi, Viazi, Shayiri na mazao mengine ya mbogamboga.