Habari

WAKULIMA WAIOMBA SERIKALI KUWAONGEZEA MAENEO YA KILIMO

WAKULIMA WAIOMBA SERIKALI KUWAONGEZEA MAENEO YA KILIMO
Jul, 26 2018

.

WAKULIMA WAIOMBA SERIKALI KUWAONGEZEA MAENEO YA KILIMO

NA; MWANDISHI MAALUM – DAKAWA

Wakulima katika eneo la Dakawa Wilayani Mvomero, wameiomba Serikali kuwaongezea eneo ambalo halitumiki kwa shughuli yoyote ile waweze kulitumia kwa kilimo cha mpunga.

Maombi hayo yametolewa baada ya kukamilika kwa ukarabati wa eneo lenye ukubwa wa hekta (2000), ambapo wananchi wamepata hamasa ya kulima baada ya kuona mafaniko ya tokanayo na kilimo cha umwagiliaji.

Akizunguma na waandishi wa habari katika skimu ya Dakawa, Mhandisi wa kanda ya Mororgoro kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Senzia Maeda, amesema Serikali kupitia Tume hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Misaada la Marekani USAID pamoja na kampuni ya SDM Smith ambayo imesanifu ukarabati wa eneo la awali imeshafanya upembuzi yakinifukwa Hekta (500) katika hizo hekta (1000) na amesema kuwamakablasha ya zabuniyapo tayari.

“Hatua inayoendelea kwa sasa ni kwa Serikali kuu kupitia Tume kutafuta mfadhili kwa ajili ya kuendeleza hilo eneo.” Alisisitiza Maeda. Na aliongeza kwa kusema kuwa Serikali ilifikia uamuzi wa kuendeleza eneo la Dakawa baada ya kuridhishwa na ukulima wa kisasa

Awali, Akiongea na waandishi wa habari Ofisini kwake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero, Bw. Florent Kyombo amesema pamoja na eneo hilo kuwa katika hatua nzuri ya uendelezwaji, Idara ya kilimo kupitia serikali ya wilaya na wataalam wa kilimo imeweza kuthibiti panya waharibifu wa mazao pamoja na ndege aina ya kwelea kwelea kwa kuharibu mazalio yao yote pamoja na suala zima la kuwasadia wakulima kupata mikopo katika baadhi ya mabenki nchini.

Bw. Arcado Ruhengiza ni mmoja wa wakilima katika skimu ya Dakawa ambapo yeye alisema kuwa endapo serikali itaongeza eneo kwa ajili ya kilimo cha mpunga, itawawezesha wakulima wengi zaidi kulima kisasa na kukuza sekta ya kilimo nchini kutokana na mafanikio waliyoyapata kupitia shamba hilo.