Mkoa wa Dodoma

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,

Mkoa wa Dodoma,

S.L.P 2957,

DODOMA.

 

  1. Utangulizi

Mkoa  wa Dodoma una Jumla ya Halmashauri saba ambazo ni; Dodoma Jiji, Chemba, Bahi  DC, Kondoa DC, Kondoa Mji, Mpwapwa DC, Chamwino DC  na  Kongwa DC. Mkoa wa Dodoma una zaidi ya hekta 51,000 zinazofaa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji. Kati ya eneo hilo, jumla ya hekta 14,003 zimeanza kuendelezwa kwa kuwekewa miundo ya kisasa ya umwagiliaji.

Hata  hivyo  msimu  wa  masika  jumla  ya  eneo  la  hekta  20,586  humwagiliwa  na kipindi  cha  kiangazi  hekta  3,145 ndizo zinazomwagiliwa.  Dodoma ina Jumla ya miradi 104 ambayo imewekewa miundo mbinu ya umwagiliaji, Uendelezaji wa miradi hii hutofautiana kiwango cha uendelevu.

Aidha kutokana na  mazingira na skimu nyingi kujengwa bila kukamilika sio  skimu  zote  zilizoendelezwa  zinafanya  kazi  kikamilifu  kufuatia kukumbwa na mafuriko na hivyo kuhitaji ukarabati mkubwa wa miundo mbinu.

Baadhi ya skimu zinazofanya kazi kwa sasa kwa kiasi za mkoa ni pamoja na Lumuma,  Kitati, Skimu za Bonde la Bahi,  Mnenia, Hombolo, Tubugwe juu, Mseta Bondeni n.k

Kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inajenga na kukarabati skimu ya Umwagiliaji Chinangali II na Mseta Bondeni na Kuchimba visima kwenye skimu ya umwagiliaji Fufu na Mvumi Makulu ili kuweza kuziongezea maji ya umwagiliaji.

Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inatarajia kujenga na kukarabati skimu za umwagiliaji kwa hatua tofauti kama kufanya Usanifu  wa skimu ( Kisese, Ngomai, e.t.c ), Ujenzi wa skimu (Membe, Msagali  Kongogo e.t.c) Kuhakiki maeneo ya umwagiliaji, Kukusanya ada na Tozo, Kutoa mafunzo kwa wakulima na  kusajili  vikundi  vya umwagiliaji katika mkoa wa Dodoma.

 

  1. Hali ya Miradi ya Umwagiliaji;

Kilimo cha umwagiliaji katika mkoa wa Dodoma unategemea kupata maji ya umwagiliaji kwa njia ya uvunaji ya maji ya mvua, Uvunaji wa maji ya ardhini, kutumia maji ya mito ya kudumu na mito ya misimu.

Miradi  mingi  inatumia  umwagiliaji  kwa  njia  ya  mtiririko  (surface irrigation  systems), aidha ni maeneo machache ambayo yanamwagilia kwa umwagiliaji wa njia ya matone (Drip irrigation systems) e.g Chinangali  II, Gawaye, Lubala na Kidoka.

 

  1.  Fursa za Umwagiliaji zilizopo Mkoa wa Dodoma.

Mkoa wa Dodoma una vigezo vingi vinavyokidhi uanzishwaji wa mashamba makubwa ya Kilimo cha umwagiliaji, vigezo hivyo ni pamoja na;

  1. Uwepo wa kiwango kikubwa cha maji ya ardhini (water table ipo juu). Maeneo mengi ya Mkoa wa Dodoma una maji mengi ardhini na Tafiti zinaonyesha kuwa asilimia hamsini ya maji yote ya Bonde la Kati yanabakia ardhnini.
  2. Uwepo wa mito ya kudumu na Mito mikubwa ya msimu
  3. Uwepo wa maeneo mazuri ya ujenzi wa mabwawa makubwa na madogo
  4. Uwepo wa mashamba makubwa yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji ambayo mengi bado hayajaendelezwa, Mkoa wa Dodoma  una maeneo mengi makubwa yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji kwa mazao mbalimbali kama vile Alizeti, Ngano, Mtama, Zabibu, Vitunguu, Mpunga n.k
  5. Utayari wa wakulima katika kuchangamkia fursa ya kilimo cha umwagiliaji
  6. Uwepo wa masoko ya Mazao ya kilimo, Dodoma kwa sasa ni makao makuu ya nchi ambayo inategewa kuwa na ongezeko kubwa la watu hivyo maitaji ya chakula yataongezeka.