Mkoa wa Kagera

TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI

TAARIFA YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI MKOA WA KAGERA

Mkoa wa Kagera ni moja kati ya Mikoa ya Tanzania inayounda Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na kutekeleza majukumu yake kama yalivyo ainishwa kwenye sheria ya Umwagiliaji Na.4 ya mwaka 2013 na Kanuni zake.

Mkoa wa Kagera kwa sasa unahudumia Wilaya nane ambazo ni Bukoba, Bukoba Vijijini, Biharamlo, Muleba, Karagwe, Kyerwa, Ngara na Misenyi.

1. FURSA ZA UMWAGILIAJI ZILIZOPO KATIKA MKOA WA KAGERA.

Kijiografia Mkoa wa Kagera una fursa kubwa ya kutumia maji ya ziwa Victoria kumwagilia Mabonde mengi makubwa yanayolizunguka Ziwa. Pia mito mingi ya Mkoa wa Kagera inatiririsha maji kwa mwaka mzima hivyo ni fursa kubwa kwa kuanzisha kilimo cha Umwagiliaji. Pia Kagera ina ardhi yenye rutuba inayokubali kila aina ya zao.

2.ORODHA YA SKIMU ZILIZOPO KATIKA MKOA WA KAGERA.

Skimu zilizoendelezwa katika Mkoa wa Kagera ni pamoja na skimu za Mwisa (Karagwe), Kyamyorwa, Kyota, Buhangaza na Buyaga (Muleba) na Kyakakera, Nkenge(Misenyi) Bigombo (Ngara) na Mwiruzi (Biharamulo).

Aidha upembuzi wa awali umefanyika katika bonde la Burigi ambapo lilitegemewa kujengwa bwawa kubwa baada ya upembuzi yakinifu na kupatikana kwa fedha. Bonde la mto Ngono (Misenyi) limefanyiwa upembuzi yakinifu kupitia Nile Basin Initiative na pindi pesa ikipatikana litaendelezwa.

Kati ya skimu zote zilizoendelezwa skimu zipatazo sita tayari zimesajiliwa ambazo ni Mwisa, Kyakakera,Buhangaza,Buyaga, Kyota na Bigombo.


 

3.ENEO LINALOMWAGILIWA KATIKA MKOA WA KAGERA.

Mapitio ya Mpango Kabambe wa Taifa wa Umwagiliaji wa mwaka 2018(Revised National Irrigation Master Plan 2018) umebainisha kuwa eneo linaloweza kumwagiliwa (Irrigation Development Potential ) katika mkoa wa Kagera  kuwa ni jumla ya hekta 90,656.80 na ambazo zimeendelezwa ni hekta 12,815.00 ambazo mgawanyo wake ni kama ilivyochambuliwa katika Jedwali Na. 1 lililoonyeshwa hapa chini. Aidha takwimu hizi zinaendelea kufanyiwa kazi ya  kuzihuisha.

PAKUA / ANGALIA PDF HAPA

Naomba Kuwasilisha

Mhandisi. Julitha Onguka

Mhandisi Umwagiliaji Kagera.