Mkoa wa Katavi

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,

S.L.P 92

Mpanda 

KATAVI

Utangulizi

Mkoa wa Katavi ulianzishwa rasmi tarehe 01 Machi, 2012 kupitia tangazo la serikali Na. 72. Mkoa una ukubwa wa eneo la kilometa za mraba 47,527 ambapo eneo la nchi kavu ni kilomita za mraba 45,843 na eneo la maji ni kilomita za mraba 1,684. Katika eneo la nchi kavu eneo lifaalo kwa Kilimo ni Hekta 932,136 na eneo la misitu ni Hekta 3,142,232. 

Serikali ya Mkoa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo imeendelea kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 katika ngazi zote za uongozi kwa kujikita zaidi katika kujenga uchumi wa Viwanda ulio imara na wa kisasa kwa ajili ya Taifa linalojitegemea na lenye maendeleo endelevu kwa wananchi wake.

Maeneo ya Utawala

Mkoa wa Katavi una jumla ya Wilaya tatu (3), ambazo ni:-

  1. Wilaya ya Mpanda,
  2. Mlele; na
  3. Tanganyika.

Pia Mkoa una Halmashauri tano (5) ambazo ni:-

  1. Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda,
  2. Halmashauri ya Mlele,
  3. Halmashauri ya Tanganyika,
  4. Halmashauri ya Nsimbo; na
  5. Halmashauri ya Mpimbwe.

Kwa ujumla Mkoa una Tarafa 10, Kata 58, Vijiji 172, Mitaa 43 na vitongoji 910.

Hali ya Hewa.

Hali ya hewa ya Mkoa wa Katavi ni kati ya nyuzi 13oc na 16oc kwa miezi ya Juni na Julai, na nyuzi 260c hadi 30oc kwa miezi ya Septemba hadi Novemba.  Kwa wastani, Mkoa hupata mvua kati ya mm 700 hadi mm 1300 zinazonyesha kati ya miezi ya Novemba mpaka Aprili.

Mkoa umegawanyika katika kanda 4 za hali ya hewa ambazo ni Bonde la Ziwa Rukwa, Nyanda za uoto wa miombo ya Katumba - Inyonga, Miinuko ya Mwese na Mwambao wa Ziwa Tanganyika

Sekta ya kilimo

Uchumi wa Mkoa wa Katavi unategemea zaidi shughuli za Sekta za Kilimo zinazochangia asilimia 90 ya pato la Mkoa na kuajiri zaidi ya asilimia 85 ya wakazi wote. Sekta za Kilimo ni pamoja na Kilimo cha Mazao, Ufugaji, Uvuvi na Ufugaji Nyuki. Mazao ya Biashara yanayolimwa ni Tumbaku, Pamba, Karanga, Korosho, Alizeti, Kahawa na Ufuta. Mazao ya Chakula ni Mahindi, Mpunga, Muhogo, Maharage, Viazi vitamu, Mtama na Ndizi.

Mifugo ifugwayo ni Ng’ombe, Mbuzi, Kondoo, Nguruwe, Kuku, Sungura na mifugo mingineyo. Shughuli za Uvuvi zinafanyika katika Ziwa Tanganyika,  Mabwawa na  Mito.

Umwagiliaji

Mkoa wa Katavi unatekeleza Kilimo cha Umwagiliaji ambacho kinatoa mchango mkubwa katika kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao ya chakula yakiwemo mpunga, mahindi, maharage na Mbogamboga ”Vitunguu n.k” , kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi Umwagiliaji umewezesha kilimo kufanyika wakati wa kiangazi, katika baadhi ya maeneo.

Eneo linalofaa kwa umwagiliaji ni jumla ya hekta 124,761 ambapo kati ya hizo eneo lililoboreshwa ni hekta 4,881, Eneo linalomwagiliwa ni jumla ya hekta 110,672 ambapo kati ya hizo hekta 105,402 zinamwagiliwa wakati wa masika na hekta 5,270 wakati wa kiangazi. 

Jedwali Namba 13: limeonesha Mchanganuo wa maeneo kwa Halmashauri:-

Mkoa wa Katavi una jumla ya skimu 33 ambapo kati ya hizo ni skimu 11 ndio zimesajiliwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

Mazao makuu yanayolimwa kwenye Skimu hizo ni pamoja na mpunga, mahindi na mbogamboga.

Jedwali lifuatalo linaonyesha mgawanyo wa skimu hizo kwa kila Halmashauri pamoja na hali zake za usajili Tume ya Taifa ya Umwagiliaji:-