Mkoa wa Manyara

MKOA WA UMWAGILIAJI WA MANYARA
MHANDISI WA UMWAGILIAJI WA MKOA
S.L.P 310
BABATI

 

                                                                                      TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI

                                                                    TAARIFA YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI MKOA WA MANYARA


Mkoa wa Manyara ni miongoni mwa Mikoa ishirini na sita (26) ya Umwagiliaji iliyo chini ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC).
Mkoa wa Manyara una jumla ya Skimu za Umwagiliaji Themanini na tisa (89) zilizoko kwenye Halmashauri saba (7) za Wilaya Tano (5), Wilaya hizo na Halmashauri zake ni kama ifuatavyo:-
1.    Wilaya ya Babati:-         a) Halmashauri ya Babati Mjini
                  b) Halmashauri ya Babati Vijijini
2.    Wilaya ya Mbulu:-         a) Halmashauri ya Mbulu Mji
b) Halmashauri ya Mbulu Vijijini
3.    Wilaya ya Hanang:-     a) Halmashauri ya Hanang
4.    Wilaya ya Simanjiro :-     a) Halmashauri ya Simanjiro
5.    Wilaya ya Kiteto:-         a) Halmashauri ya Kiteto
Mkoa wa Manyara una jumla ya eneo la hekta 37,314 linalofaa kwa ajili ya kilimo cha Umwagiliaji, eneo lililosanifiwa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Umwagiliaji ni hekta 20,317 wakati eneo lililoendelezwa ni hekta 10,777 na eneo linalomwagiliwa kwa njia za asili ni hekari 12,230 hivyo kufanya eneo lote linalolimwa kwa kilimo cha Umwagiliaji kuwa na jumla ya hekari 23,007.
Kati ya Skimu themanini na tisa (89) zilizopo Mkoani Manyara, Skimu kumi (10) zinamilikiwa na watu binafsi na Skimu kumi na sita (16) ndizo zilizosajiliwa chini ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji. Jumla ya wakulima katika Skimu sabini na tisa (79) zinazomilikiwa na wananchi ni 12,332 kati yao wanawake ni 2891 na wanaume ni 9441.
Vyanzo vya maji katika Mkoa wa Manyara ni vya uhakika ikiwa ni pamoja na mito ya kudumu inayotiririsha maji kwa mwaka mzima, chemchem zisizokauka, maziwa ya maji pamoja na mabwawa. Mito ya kudumu ni Mto Bermi, Kiongozi, Yaeda, Nambij, Bubu, Mangisa, Tumati, Dudumera, Magara, Shauri moyo na Pangani/Ruvu. Maziwa yaliyopo Mkoani Manyara ni ziwa Manyara na ziwa Babati na ziwa Manyara.
Mazao makuu yanayolimwa kwenye Skimu za Umwagiliaji Mkoa wa Manyara ni Mpunga, Vitunguu saumu, Vitunguu maji, Mahindi, Maharage, Miwa na Mbogamboga.
Wastani wa uzalishaji wa mazao Mkoa wa Manyara ni kama ifuatavyo:-
a)    Mpunga ni tani saba (7) kwa hekta
b)    Vitunguu saumu ni tani saba na nusu (7.5) kwa hekta
c)    Vitunguu maji ni tani kumi (10) kwa hekta
d)    Mbogamboga ni tani kumi (10) kwa hekta
e)    Mahindi ni tani nne (4) kwa hekta
f)    Maharage ni tani tano (5) kwa hekta