Mkoa wa Ruvuma

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,

Mkoa wa Ruvuma,

S.L.P 74,

RUVUMA.

TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI MKOA WA RUVUMA

MPANGO KAZI

JULAI 2022 – JUNI 2023

 

Shughuli: Ukarabati wa miradi ya umwagiliaji ambayo haifanyi kazi katika skimu 16.

Changamoto: Ufinyu wa bajeti katika uakrabati na ukamilishaji wa ujenzi.

Mpango Na.1:  Ili kutekeleza shughuli hizi serikali kuu na  Halmashauri za Wilaya zitenge bajeti na kuzielekeza katika maeneo husika kwa    wakati.

Mpango Na.2:  Miradi itajenwa kwa kuwatumia mafundi wenye taalumu kwa usimamizi wa wahandisi.

Shughuli: Ukusanyaji wa tozo katika skimu 16 zilizojengwa miundombinu ya umwagiliaji.

Changamoto: Fedha kwa  ajili ya utekelezaji wa kazi .

Mpango Mkakati Na. 1: Kushirikisha Halmashauri za Wilaya pamoja na Vyama vya Umwagiliaji kuhusu umuhimu wa kutoa tozo.

Mpango No. 2: Kuvijengea uwezo vyama vya wakulima wa umwagiliaji ili viweze kuwa na uwezo wa kukusanya tozo.

Shughuli:Usajili wa skimu za Umwagiliaji.

Changamoto: Upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa kazi.

Mpango Na. 1: Kushirikisha Maafisa kilimo wa Wilaya na Vyama vya wakulima wa Umwagiliaji kuhusu umuhimu wa usajili wa skimu chini ya sheria na. 4, 2013 ya Umwagiliaji. 

Mpango Na. 2: Kuzipitia skimu zote zilizosajiliwa katika usajili wa zamani (Wizara ya mambo ya ndani) na kushauliana na vyama vya wakulima wa umwagiliaji kusajili upya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji iliyopo chini ya Wizara ya kilimo.

Shughuli: Utambuzi wa maeneo yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji.

Changamoto: Upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa kazi.

Mpango: Kuongeza eneo linalofa kwa kilimo cha umwagiliaji ili mkoa uweze kuwa na uhakika wa chakula .

Shughuli: Utoaji wa elimu kwa wakulima wa umwagiliaji kuhusu uendeshaji na matunzo ya miundombinu.

Changamoto: Upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utoaji mafunzo.

Mpango: Kuzifikia skimu zote zilizojengewa miundombinu ya umwagiliaji katika kuzijengea uwezo.

Shughuli: Ushirikishwaji wa wakulima wa umwagiliaji katika kuyatambua maeneo wanayolima ndani ya skimu.

Changamoto: Upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa kazi ya utambuzi wa wakulima na ukubwa wa maeneo wanayamiliki.

Mpango: Kutambua ukubwa wa maeneo kwa kila mkulima anayelima katika skimu ili kurahisiha utoaji wa huduma za kitaalamu, kibenki na ukusanyaji wa tozo mbalimbali za umwagiliaji kulingana na Sheria Na. 4, 2013 ya Umwagiliaji.

Shughuli: Ufuatiliaji na tathimini shirikishi katika skimu zote zilizorabatiwa na kujengewa miundombinu.

Changamoto: Upatikanaji wa fedha kwa ajili ya ufuatiliaji na tahimini.

Mpango: Kufanya ufuatiliaji kwa skimu zote zitakazo karabatiwa na kujengewa miundombinu.

Shughuli: Kupanda miti katika vyanzo vya maji ili kuhifadhi mazingira.

Changamoto: Upatikanaji wa fedha kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira.

Mpango: Kushirikisha vyama vya wakulima wa umwagiliaji kuhusu utunzaji wa mazingira.