Mkoa wa Singida

TAARIFA FUPI

  1. HALMASHAURI ZILIZOPO MKOA WA SINGIDA

Mkoa wa Singida una hakmashauri saba(7),ambazo ni

  1. Singida Manispaa
  2. Singida vijijini
  3. Iramba
  4. Mkalama
  5. Manyoni
  6. Ikungi
  7. Itigi

2.0 FURSA ZA UMWAGILIAJI ZILIZOPO MKOA WA SINGIDA

Mkoa wa Singida unafursa mbalimbali kwenye kilimo cha umwagiliaji, maeneo hayo ni pamoja na;

  1. Uwepo wa mashamba makubwa yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji, Mkoa wa Singida una maeneo mengi makubwa yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji kwa mazao mbalimbali kama vile vitunguu,mpunga n.k
  2. Uwepo wa mito mikubwa ya mvua ambayo pamoja na kwamba ni ya msimu lakini inatiririsha maji mengi kiasi kwamba maji hayo yakivunwa yatakuwa ni fursa kubwa sana kwa wakulima.
  3. Uwepo wa kiwango kikubwa cha maji ya kuchimba kwa njia ya visima virefu vya kuchimba(water table ipo juu),kwa sehemu kubwa maeneo mengi ya Singida yana maji mengi(ground water) maji ambayo yanaweza kutumika kwa kilimo cha umwagiliaji.
  4. Utayari wa wakulima katika kuchangamkia fursa ya kilimo cha umwagiliaji, sehemu kubwa ya mkoa wa Singida imezungukwa na mchanganyiko wa makabila mbalimbali ambayo yana utayari mkubwa wa kulima endapo patakuwa na uhakka wa vyanzo vya kudumu vya maji.
  5. Uwepo wa skimu iliyo karibu na mgodi eneo hili ni fursa kubwa kwa wakulima kwani uwepo wa mradi wa uhakika utasababisha uwepo wa soko la uhakika kutoka mgodini,jambo ambalo litasaidia sana katika kukuza kipato cha mkulima mmoja mmoja.(Skimu inahitaji uendelezaji)

3.0 ORODHA YA SKIMU ZILIZOPO MKOA WA SINGIDA

Mkoa wa Singida una skimu za aina nne,

  1. Skimu zilizoendelezwa na zinafanya kazi masika na kiangazi ( Jedwali Na.1)
  2.  skimu zilizoendelezwa kwa kujengewa banio na zinafanya kazi masika tu(Jedwali Na.2)
  3. Skimu ambazo hazijafanyiwa uendelezaji wowote na zinafanya kazi kwa kiwango cha chini(Jedwali Na.3)
  4. Skimu zilizoendelezwa na hazifanyi kazi kutokana na athari ya mvua(Jedwali Na.4)

4.0 ENEO LINALOMWAGILIA

Eneo Linalofaa (ha) Eneo linalomwagiliwa masika (ha) Eneo linalomwagiliwa kiangazi (ha)
48,619 17,437.6 293.6

5.0 VYANZO VYA MAJI VILIVYOPO MKOA WA SINGIDA

Mkoa wa  Singida una vyanzo mbalimbali vya maji kama ifuatavyo;

  1. Mabwawa
  2. Mito ya msimu
  3. Visima virefu
  4. Maziwa madogo madogo