Usimamizi wa Mazingira na Kijamii

Madhumuni

Kushughulikia masuala yanayohusu mazingira katika mifumo ya umwagiliaji na matupio ili kuhakikisha uendelevu.

Kitengo hikikitafanya kazi zifuatazo:-

(i) Kuandaa tathmini ya awali ya hifadhi ya Mazingira na Jamii;

(ii) Kuwezesha na kuratibu tathmini ya awali ya athari za kimazingira kwa ajili ya kuendeleza umwagiliaji na Matupio;

(iii) Kufanya ukaguzi wa masuala ya mazingira na jamii kwenye katika shughuli za umwagiliaji naMatupio;

(iv) Kuhakikisha masuala yanayohusu mazingira na jamii yanazingatiwa katika mipango ya umwagiliaji na matupio, usanifu na utekelezaji wake;

(v) Kuratibu shughuli zinazohusiana na mazingira ndani ya Tume;

(vi) Kuandaa na kuratibu utekelezaji wa mipango ya usimamizi wa mazingira na jamii katika skimu za umwagiliaji; na

(vii) Kutoa ushauri wa kimazingira na Jamii na uwezeshaji wa kitaalam kwa wafanyakazi wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka ya Serikli za Mitaa wanaofanya kazi katika sekta ya Umwagiliaji.

Kitengo hiki kitaongozwa na Afisa Mazingira Mkuu