Fedha na Akaunti
Madhumuni
Kutoa huduma ya usimamizi wa masuala ya fedha na vitabu vya mahesabu ya fedha za Tume.
Kitengo hiki kitafanya kazi zifuatazo:-
Mishahara
(i) Kuandaa malipo ya Mishahara ikiwemo makato yakisheria;
(ii) Usimamizi wa malipo ya mishahara;
(iii) Kuandaa makisio ya masilahi ya watumishi;
(iv) Kuandaa Nyaraka za Pensheni; na
(v) Kutunza Kumbumbuku.
Ofisi ya malipo
(i) Kupeleka orodha ya nyaraka za malipoHazina;
(ii) Kuchukua hundi zote kutoka Hazina;
(iii) Kupeleka benki malipo ya fedha taslimu na hundi;
(iv) Kutayarisha taarifa ya fedha ya kila mwezi;
(v) Kuwalipa watumishi/wateja (watoa huduma) fedha taslimu au hundi;
(vi) Kutunza kwenye vitita vocha za malipo yaliyofanyika;
(vii) Kutunza vitabu vya malipo ya fedha taslimu;
(viii) Kutunza/kuwianisha malipo ya safari yaliyoidhinishwa; na
(ix) Kuandaa na kulipa malipo yote.
Mapato
(i) Kukusanya mapato yote;
(ii) Kusimamia mapato kulingana na kanuni na miongozo; na
(iii) Kufanya usiluhisho wa hesabu za Tume katika benki.
Penshseni
(i) Kuandaa Nyaraka za pensheni; na
(ii) Kutunza kumbukumbu za pensheni.
Bajeti
(i) Kuandaa bajeti;
(ii) Kufuatilia mgawanyo na matumizi;
(iii) Kuandaa hesabu za mwisho wa mwaka na taarifa nyinginezo zakifedha.
Ukaguzi waHesabu wa Awali
(i) Kukagua nyaraka za malipo ikiwa ni pamoja na idhini kulingana na taratibu;
(ii) Kukagua taratibu za kifedha na kuhakikisha zinaendana na sheria, kanuni, Nyaraka mbalimbali; na
(iii) Kujibu hoja zote za ukaguzi kwakipindi cha mwaka wa fedha uliopita.
Kitengo hiki kitaongozwa na Mhasibu Mkuu