Mawasiliano ya Serikali
Madhumuni
Kutoa utaalamu , huduma ya habari na mawasiliano kwa Tume; na kufanya majadiliano na umma na vyombo ya habari.
Kitengo hiki kitafanya kazi zifuatazo:-
(i) Kuandaa na kusambaza nyaraka kama vipeperushi, machapisho, makala za magazeti na kutaarifu umma juu ya sera, programu, majukumu na mageuzi yanayofanywa na Tume;
(ii) Kuratibu utoaji wa habari kwa ajili ya Tume;
(iii) Kushiriki katika mazungumzo na umma ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari juu ya masuala yanayohusu Tume;
(iv) Kuendeleza programu za Ofisi;
(v) Kuratibu uandaaji wa machapisho ya Tume kwa ajili ya semina na mikutano;
(vi) Kuratibu uandaaji na uzalishaji wa machapisho na magazeti;
(vii) Kuboresha taarifa za ofisi kwenye tovuti ya Tume;
(viii) Kushauri juu ya uandaaji wa nyaraka mbalimbali; na
(ix) Kuandaa na kutekeleza mkakati wa mawasiliano wa Tume.
Kitengo hiki kitaongozwa na Afisa Habari Mkuu.