Teknolojia Habari na Mawasiliano
Madhumuni
Kutoa utaalamu na huduma juu ya matumizi ya TEHAMA kwa Tume.
Kitengo hiki kitafanya kazi zifuatazo:-
(i) Kutekeleza sera ya TEHAMA na Serikali-Mtandao;
(ii) Kuandaa na kuratibu mifumo ya usimamizi wa habari shirikishi katika Tume;
(iii) Kuhakikisha vifaa vya kompyuta na programu vinatunzwa vizuri;(iv) Kuratibu na kusaidia taratibu za manunuzi ya vifaa vya kompyuta na programukatika Tume;
(v) Kubuni, kuendeleza na kutekeleza udhibiti na kuhakikishausalama, uadilifu na upatikanaji wa habari;
(vi) Kuanzisha na kuratibu matumizi ya mawasiliano ya mtandao katika eneo husika (LAN and WAN); na
(vii) Kuandaa mafunzo na kupendekeza maeneo ya matumizi ya TEHAMA kama chombo cha kuboresha utoaji wa huduma katika ofisi yote.
Kitengo hikikitaongozwa na Mchambuzi wa Mifumo ya Compyuta Mkuu.