Ukaguzi wa Ndani

Madhumuni

Kutoa huduma zenyeuhakikana ushauri kwa Mkurugenzi Mkuu katika usimamizi bora wa Rasilimali fedha.

Kitengo hiki kitafanya kazi zifuatazo:-

(i) Kufanya mapitio na kutoa taarifa juu ya udhibiti sahihi wa mapokezi, uhifadhi na matumizi ya rasilimali fedha za Tume;

(ii) Kufanya mapitio na kutoa taarifa juu ya uzingatiaji wa taratibu za fedha zilizowekwa kwenye sheria ama kanuni au maagizo ya udhibiti wa matumizi ya fedha za Tume;

(iii) Kufanya mapitio na kutoa taarifa juu ya uainishaji na mgawanyo sahihi wa mapato na matumizi ya kihasibu; na

(iv) Kuandaa taratibu za kiukaguzi kulingana na Viwango vya Kimataifa;

(v) Kufanya mapitio na kutoa taarifa juu ya usahihi na ukweli wa kifedha na matumizi ya takwimu na kuandaa taarifa za kifedha na nyinginezo;

(vi) Kufanya mapitio na kutoa taarifa juu ya mfumo unaotumika kutunza rasilimali na kuhakiki uwepo wa rasilimali hizo;

(vii) Kufanya mapitio na kutoa taarifa juu ya utendaji au mipango ya kuhakiki ikiwa matokeo yanaendana na malengo na madhumuni yaliyokusudiwa;

(viii) Kufanya mapitio na kutoa taarifa juu ya maelezo ya Menejementiya Tume kwa ukaguzi wa ndani, nje, na taarifa ya tathmini ya nje na kuisaidia Menejeminti katika kutekeleza mapendekezo;

(ix) Kufanya mapitio na kutoa taarifa juu ya utoshelevu wa udhibiti wa mfumo wa kompyuta uliojengwa ndani ya Tume;

(x) Kutoa uhakika na huduma za ushauri wa namna ya kusimamia athari na michakatoya utawala bora;

(xi) Kuandaa mikataba ya huduma kwawateja juu ya shughuli za ukaguzi wa ndani na kamati ya ukaguzi.

(xii) Kuandaa mpango-mkakati wa kiukaguzi

Kitengo hiki kitaongozwa na Mkaguzi Mkuu wa ndani