Huduma za Kisheria

Madhumuni

Kutoa utaalamu nahuduma za kisheria kwa Tume.

Kitengo hiki kitafanya kazi zifuatazo:-

(i) Kutoa ushauri wa kisheria na usaidizi kwa Idara na Vitengo vya Tume juu ya tafsiri za sheria, masharti yamikataba, masharti yamakubaliano, masharti ya ubinafsishaji, mikataba ya manunuzi, udhamini, barua za ahadi, mkataba wa makubaliano, makubaliano ya ushauri na aina nyingine za makubaliano na nyaraka nyingine za kisheria;

(ii) Kutoa ushauri wa kitaalamu katika kuandaa nyaraka za kisheria zikiwemo sheria zilizopitishwa na Bunge na sheria ndogo, na kuziwasilisha ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali;

(iii) Kusimamia mazungumzo ya kazi na makubaliano ya maendeleo ya ajira;

(iv) Kushiriki katika majadiliano na mikutano mbalimbali inayohusu utaalamu wa kisheria juu ya kazi na sekta za ajira;

(v) Kutafsiri sheria na kanunindani ya Tume;

(vi) Kuwasiliana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali juu ya kesi za madai, jinai na madai mengine yanayohusu Tume; na

(vii) Kutoa ushauri wa kiutaalamu kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali juu ya kupitia nyaraka mbalimbali za kisheria kama vile maagizo, taarifa, vyeti na makubaliano na uhamishaji wa umiliki.

Kitengo hiki kitaongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu