Usimamizi wa Manunuzi
Madhumuni
Kutoa utaalamu nahuduma juu ya manunuzi, utunzaji, ugavi wa bidhaa na huduma, na ufutaji wa mali chakavuza Tume.
Kitengohiki kitafanya kazi zifuatazo:-
(i) Kuishauri Menejemintijuu ya masuala yanayohusu manunuzi ya bidhaa na huduma, mbinu za usimamizi na ufutaji wa mali chakavu;
(ii) Kufuatilia uzingatiaji wa mchakato wa manunuzi na taratibu kwa mujibu wa sheria ya manunuzi na kanuni zake;
(iii) Kuandaampango wa manunuzi wa mwaka wa Tume;
(iv) Kufanya manunuzi na kufuta vifaa chakavu,kutunza na kusimamia ugavi, vifaa na huduma za kuendesha shughuli za Tume;
(v) Kutunza na kufuatilia mgawanyo wa mahitaji ya ofisi na vifaa;
(vi) Kutunza na kuboresha orodha ya bidhaa, mahitaji na vifaa;
(vii) Kutoa huduma za sekretarieti kwenye bodi ya manunuzi kwa mujibu wa sheria ya manunuzi na kanuni zake;
(viii) Kuainisha viwango/vipimo vya bidhaa na huduma zinazonunuliwa na kuhakikisha kuwa vinazingatiwa; na
(ix) Kuandaampango kazi, bajeti, nataarifa za utekelezaji wa kitengo.
Kitengo hiki itaongozwa na Afisa Ugavi Mkuu.