

Picha inayoonyesha maendeleo ya ujenzi wa Bwawa la Membe Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma linalo tarajiwa kumwagilia skimu zenye jumla ya Hekari 8000 mara litakapo kamilika.

Mhe, Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan akipanda mti katika eneo la uzinduzi wa mashamba makubwa ya umwagiliaji (Block Farm) Chinangali Dodoma, (aliyevaa kofia) ni Waziri wa Kilimo Mhe, Hussein Bashe na (aliyevaa miwani) ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw, Raymond Mndolwa.

Mhe. Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan akizindua mashamba makubwa ya umwagiliaji (Block Farm) katika eneo la Chinangali nje kidogo ya mji wa Dodoma. Wanaoshuhudia zoezi hilo kushoto kwa Rais Samia ni Spika wa Bunge Mhe, Dkt. Tulia Ackson. (aliyevaa Kofia ni Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe. (Aliyevaa miwani ) ni Waziri Mkuu Mstaafu Peter Pinda.

Waziri wa Kilimo Mhe, Hussein Bashe amesema, Hadi tarehe 20 april 2023, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inatekeleza miradi 48 kati ya 69 sawa na asilimia 70% ya miradi ya umwagiliaji katika bajeti ya mwaka 2022 -2023, shilingi Bilioni 85 kati ya Bilioni 234 zimetumika kuwalipa wakandarasi.

Picha ya pamoja baina ya Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe, Wajumbe wa Bodi ya Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na baadhi ya Wakurugenzi wa Kampuni zinazojenga Miradi ya Umwagiliaji. Jijini Dodoma.

Picha inaonyesha mashamba ya mpunga kwa umwagiliaji katika Skimu ya Umwagiliaji Rungwe Mpya, wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.