Habari
BASHE, ATETA NA WAHANDISI WA MIKOA WA UMWAGILIAJI

📍NIRC Dodoma
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb), amefanya kikao kazi na Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) inayoongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Bw. Raymond Mndolwa, pamoja na Wahandisi wa Umwagiliaji kutoka mikoa mbalimbali.
Kikao hicho, kilichofanyika jijini Dodoma, kililenga kuboresha utendaji na kuongeza ufanisi katika sekta ya Umwagiliaji. Pia kilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayesimamia Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula, Dkt. Hussein Mohamed Omar.
Mbali na kujadili masuala ya kiutendaji, kikao hicho kilitazama njia za kukuza ushirikiano na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo ili kuhakikisha malengo ya Wizara na Serikali yanafikiwa.
Miongoni mwa malengo hayo ni utoaji wa huduma bora kwa wakulima, kuongeza uzalishaji wa chakula, kufanikisha kujitosheleza kwa chakula ndani ya nchi, kuwa na akiba ya kutosha, pamoja na kuuza chakula nje ya nchi.