Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji

Habari

BODI YA NIRC YAHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI



📍 NIRC Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Dkt. Richard Masika amewataka wajumbe wa Bodi hiyo na Uongozi wa Tume kuzingati uwajibikaji lengo ni kuleta matokeo sekta ya kilimo.

Dkt. Masika ametoa kauli hiyo wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa wajumbe wa Bodi na baadhi ya wajumbe wa Menejiment ya Tume ambapo amesisitiza haja ya uongozi kuwajibika ili kuleta matokeo.

Amesema hatua ya kutekeleza kwa vitendo mafunzo waliyopatiwa ni muhimu hususani katika kuisimamia Bodi hiyo kwa weledi na kuleta matokeo chanya katika sekta ya kilimo cha Umwagiliaji nchini.

 


“Mafunzo haya yamelenga kukumbusha wajibu wa Bodi kwa Tume, uongozi, sifa na wajibu wa viongozi.

“Ni muhimu wajumbe wa Bodi tutambue kuwa hatupo hapa kwa kubahatisha bali Tume inahitaji uwajibikaji na mshikamano ili kufanikisha dira ya Tume kwa manufaa ya Taifa,”amesisitiza.

Amesema kuwa mafunzo hayo yameweka misingi thabiti kwa uongozi wa Tume na Bodi kwa ujumla.



Aidha ameitaka Menejiment kuandaa mafunzo kwa watumishi na kubadikishana uzoefu waliopata katika mafunzo hayo ili kukumbusha wajibu wao katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.



Kwa upande wake Mwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Huria Dkt. Emanuel Mallya, amesema ushiriki wa Bodi na Menejiment katika mafunzo hayo, utaleta matokeo chanya kwa kuwa utaongeza tija katika usimamizi wa kazi za taasisi hiyo na kufikia malengo yaliyopo.

Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa Menejimenti walioshiriki mafunzo hayo Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Andrew Rugarabamu amesema mafunzo hayo yataongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku na kuleta matokeo chanya katika maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.