Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb), afanya kikao kazi na Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) inayoongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Bw. Raymond Mndolwa, pamoja na Wahandisi wa Umwagiliaji wa mikoa, kikiwa na lengo ni kuboresha utendaji na kuleta ufanisi katika sekta ya Umwagiliaji ambapo pia kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayesimamia Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula, Dkt. Hussein Mohamed Omar.